Home LOCAL NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI

NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI

Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na mwandishi wa kitabu hicho Wakili Ally Kileo pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kitabu hicho.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akionesha kitabu alichokizindua chenye kurasa Zaidi ya 900. Kulia kwake ni mwandishi wa kitabu hicho Wakili Ally Kileo na kushoto ni Prof. Chris Peter Maina.

Wakili Ally Kileo ikimkabidhi Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro zawadi mara baada ya kukamilisha kazi ya uzinduzi wa kitabu hicho.

Na: Lusajo Mwakabuku – WKS Dar es Salaam.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua kitabu cha masuala ya ajira na sheria za kazi chenye kurasa zaidi ya Mia Tisa jijini Dar es salaam na kuwataka watanzania wengine kujikita katika kuandika vitabu hasa vyenye uchambuzi wa kisheria ambavyo vitawaongezea uelewa watanzania juu ya sheria zao na haki wanazostahili.

Waziri Ndumbaro ameyasema hayo usiku wa jana Tarehe 25/01/2023 alipoalikwa kama Mgeni Rasmi katika Hotel ya Johari Rotana kuzindua kitabu hicho kilichoandikwa na Wakili Msomi bwana Ally Kileo na kuongeza kuwa kitabu hiki kimegusa kila eneo muhimu katika mazingira ya ajira yakiwemo masuala ya haki za kunyonyesha na ni kwa kiasi gani sheria hiyo inatakelezwa katika nchi yetu.

“Hiki ni kitabu changu cha Tano sasa kukizindua lakini katika vitabu vyote vinavyohusiana na masuala ya sheria hapa nchini hiki ni kitabu cha kwanza ambacho nimekiona kinaunganisha moja kwa moja suala la ajira na haki ya mama kunyonyesha” Alisema Ndumbaro.

Aidha Waziri Ndumbaro alisema kitabu hiki kimegusa maeneo muhimu kama vile sheria za uwekezaji zinavyotekelezwa hapa nchini na kuongeza kuwa kabla mwekezaji hajaamua sehemu ya kuwekeza, moja ya vitu muhimu anavyoangalia ni sheria za ajira ili kuepusha mikwaruzano kati yake na  serikali, hivyo kitabu hiki kitarahisisha taratibu za masuala ya uwekezaji kwani kinaelezea na kufafanua masuala yote muhimu yanayohusiana na sheria hizo sehemu za kazi.

Wakielezea kwa nyakati tofauti mapitio ya kitabu hicho, Prof. Chris Peter Mahina alisema kitabu hicho kimelenga kumfanya mtanzania kupambania haki zake katika maeneo mbalimbali ya ajira huku Dkt. Dominucus Makukula  akielezea namna vyombo vya Habari vinavyosaidia ama kuvuruga pale ambapo mahusiano ya ajira kati ya muajiri na muajiriwa yanapoharibika.

Wakili Ally Kileo wakati akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisema kitabu chake chenye kurasa 941 na sura 20 kimemchukua Miaka Mitano kukikamilisha na kinapatikana kwa nakala ngumu (hard copy) na laini (softcopy).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here