Home LOCAL SERIKALI KUSHIRIKISHA JAMII FAIDA ZA BIMA YA AFYA KWA WOTE

SERIKALI KUSHIRIKISHA JAMII FAIDA ZA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Mratibu wa Mawasiliano ya afya na mabadiliko ya tabia katika jamii ,Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Peter Mabwe akifunga kikao cha kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii[CBHP-TAC Meeting] chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii  kilichoratibiwa na  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT   -Tanzania na BMF.

Afisa Program huduma za afya ngazi ya jamii ,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya Orsolina Tolage akiwasilisha mada umuhimu wa ushirikishwaji kwa jamii katika afua mbalimbali za Afya .

Afisa Mwezeshaji wa Mafunzo ya watoa huduma ngazi ya Jamii kitaifa ,John Yuda akizungumza katika   kikao cha kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii[CBHP-TAC Meeting] chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii  kilichoratibiwa na  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT   -Tanzania na BMF.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii[CBHP-TAC Meeting]  wakishiriki kwenye kikao chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii  kilichoratibiwa na  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT   -Tanzania na BMF.

Na: Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga ,Wizara ya Afya.

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma imesema itaendelea kushirikisha jamii faida za Bima ya Afya kwa Wote pamoja na afua mbalimbali za afya.

Hayo yamebainishwa mkoani Morogoro na Mratibu wa Mawasiliano ya afya na mabadiliko ya tabia katika jamii ,Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Peter Mabwe wakati akifunga kikao cha kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii[CBHP-TAC Meeting] chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii  kilichoratibiwa na  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT   -Tanzania na BMF.

Mabwe amesema ushirikishwaji  katika  uboreshaji wa huduma ngazi ya jamii ikiwemo umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote ni muhimu katika kuimarisha huduma za afya nchini .

“Ushirikishwaji kwa jamii katika faida za Bima ya Afya Wote ni muhimu watumishi sekta ya afya na wadau kuendelea kutoa elimu hii kwani Bima ya afya kwa wote itahakikisha kila Mtanzania anapata matibabu kila kujali kipato chake hali itakayosaidia kupata matokeo mazuri kuboresha huduma za afya kwa mwananchi”amesema Mabwe.

Aidha,Mabwe  amesema Bima ya Afya kwa Wote itasaidia katika utoaji wa huduma za afya katika idara ya Kinga  na kusaidia kupata matokeo mazuri katika afya ya kila Mwananchi.

Ikumbukwe kuwa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote unatarajiwa kusomwa Bungeni hivi karibuni na ukipitishwa utaanza kufanya kazi rasmi Mwezi Julai,2023 na itarahisisha ubora wa huduma na kila mwananchi kuwa na uhakika wa kupata matibabu.

MWISHO.

 

Previous articleSERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA UPANDIKIZAJI WA MIMBA KUPITIA BIMA YA AFYA KWA WOTE
Next articleNDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here