Home BUSINESS BoT YABAINI KUONGEZEKA KWA UDANGANYIFU WA MIAMALA YA FEDHA MTANDANI

BoT YABAINI KUONGEZEKA KWA UDANGANYIFU WA MIAMALA YA FEDHA MTANDANI

Benki Kuu ya Tanzania imebaini kuongezeka kwa udanganyifu wa fedha nchini unaohusisha mwananchi kupokea taarifa (hati au barua pepe) inayodai kuwa ni uthibitisho wa malipo kupitia SWIFT na/au mifumo mingine ya uhamishaji fedha.

Mpokeaji anafahamishwa kuwa fedha zimeingizwa kwenye benki au akaunti katika taasisi ya fedha nchini Tanzania; wakati mwingine, mpokeaji fedha anaelekezwa kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha hizo nyingi.

Matukio mengi ya taarifa hizo yanahusisha kiasi kikubwa cha pesa kinachodaiwa kuletwa kwa ajili ya ufadhili wa mradi au matumizi binafsi. Hivyo, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo ni za kughushi na za kubuni.

Wananchi mnashauriwa kuwa waangalifu na kuacha kujihusisha na miamala hiyo ambayo kwa kawaida inalenga kuwatapeli fedha. Pia, wananchi mnakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kufanya miamala ya fedha ili kuepuka upotevu wa fedha ambazo ni:

i. Kuhakikisha usalama wa taarifa za fedha wakati wa kutoa taarifa binafsi mtandaoni (tovuti, mitandao ya kijamii), kupitia barua pepe au kwenye simu;

ii. kutojihusisha kujibu barua pepe, barua au simu zinazoahidi kupokea fedha kutoka kwa watu au kampuni wasizozifahamu vizuri; na

iii. kuwa waangalifu mnapofanya malipo ya mtandaoni kwa kufanya uhakiki wa mshirika wa kibiashara (mtu au kampuni) kabla ya kutoa maelezo au kufanya malipo.

Aidha, wananchi waliokumbwa na matatizo hayo wanashauriwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama kwa hatua stahiki.

  BENKI KUU YA TANZANI

Previous articleWAZIRI MKUU ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI HOSPITALI YA NAMTUMBO
Next articleWAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SEKONDARI YA WASICHANA YA DKT.SAMIA SULUHU HASSAN, RUVUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here