Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Mwalim Ali Mwalim akifungua kikao cha kikao cha kawaida cha robo ya pili cha Baraza la Michezo kwa wajumbe walishiriki katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi Mwanakwerekwe Magharib “B” Mjini Zanzibar.
Na: Miza Othman- (BTMZ). 20 /01/2023.
Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar limeona ipo haja ya kutumia mbinu mbadala ya kuwashawishi vijana katika kushiriki michezo mbalimbali kwani kufanya hivyo kutaondokana na wimbi kubwa la vijana kujishirikisha na vikundi viovu na kutapelekea kukuza maendeleo ya Taifa Nchini kwao.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Ndugu Mwalim Ali Mwalim aliyasema hayo wakati walipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza katika kikao cha kawaida cha robo ya pili cha Baraza la Michezo kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B” Unguja.
Alisema ni vyema Wajumbe wa Baraza hilo kuwa makini katika kutekeleza majukumu ya kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia kurahisisha usimamiaji na uendelezaji wa shughuli za michezo hapa Zanzibar.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema upo muhimu wa sekta ya michezo kupewa kipaombele kwani sekta hiyo inasaidia kuwanyanyua vijana kuondokana na utegemezi katika kujikwamua Maisha yao na kulinyanua taifa kiuchumi .
“Hakuna mtu yeyote anaweza kushawishiwa kuingia ndani ya michezo kwani ni maamuzi ya mtu mwenyewe kushiriki mfano wachezaji kama Pele, Bekam kutokana hivi sasa wanapata fursa za kushiriki maamuzi ya vikao mbalimbali katika taifa”, Alisema Mwenyekiti.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine alisema Baraza la Michezo limeona upo umuhimu wa kuanzisha tamasha la michezo litakazoweza kuwainua vijana na kuonyesha vipaji walivyonayo kwa kuonekana ndani ya mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Hata hivyo aliwataka wajumbe hao kushiriki katika vikao mbalimbali vinavyojadiliwa na kuweza kubuni mambo yatakayowawezesha kuibuwa njia za kukuza michezo hapa nchini kwao.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho walisema ni vyema kuandaa kanuni na sheria na kufanyiwa kazi kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha utekelezaji wa kazi zao kwa uhakika.