Home SPORTS BARAZA LA TAIFA LA MICHEZO ZANZIBAR

BARAZA LA TAIFA LA MICHEZO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Mwalim Ali Mwalim  akifungua kikao cha kikao cha kawaida cha robo ya pili  cha Baraza la Michezo kwa wajumbe walishiriki katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi   Mwanakwerekwe Magharib “B” Mjini Zanzibar. 

Na: Miza Othman- (BTMZ).  20 /01/2023.

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar  limeona ipo haja ya  kutumia mbinu mbadala ya kuwashawishi vijana  katika kushiriki michezo mbalimbali  kwani kufanya hivyo  kutaondokana na wimbi kubwa la vijana  kujishirikisha na vikundi viovu na kutapelekea kukuza maendeleo ya Taifa  Nchini kwao.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Ndugu  Mwalim Ali Mwalim  aliyasema hayo wakati walipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza katika kikao cha kawaida cha robo ya pili  cha Baraza la Michezo kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya  Magharib “B” Unguja.

Alisema ni vyema Wajumbe wa Baraza hilo  kuwa makini katika kutekeleza majukumu ya kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia  kurahisisha usimamiaji na uendelezaji wa shughuli za michezo hapa Zanzibar.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema upo muhimu wa sekta ya michezo kupewa kipaombele  kwani sekta hiyo  inasaidia  kuwanyanyua vijana kuondokana na utegemezi katika kujikwamua Maisha yao na  kulinyanua taifa kiuchumi .

“Hakuna mtu yeyote anaweza kushawishiwa kuingia ndani ya michezo kwani ni maamuzi ya mtu mwenyewe kushiriki mfano wachezaji kama Pele, Bekam kutokana hivi sasa wanapata fursa za kushiriki maamuzi ya vikao mbalimbali katika taifa”, Alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine alisema Baraza la Michezo  limeona upo umuhimu wa kuanzisha tamasha la michezo litakazoweza kuwainua vijana na kuonyesha vipaji walivyonayo kwa  kuonekana ndani ya mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Hata hivyo aliwataka wajumbe hao kushiriki katika vikao mbalimbali vinavyojadiliwa na kuweza kubuni mambo yatakayowawezesha kuibuwa njia za kukuza michezo hapa nchini kwao.

 Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho walisema ni vyema  kuandaa kanuni na  sheria na kufanyiwa kazi  kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha utekelezaji wa  kazi zao kwa uhakika.

Previous articleWAZIRI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE AWAPONGEZA  WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE SHERIA
Next articleWASIMAMIZI WA ELIMU WAKUTANA KUJADILI MIPANGO YA KUBORESHA ELIMU SHINYANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here