Home LOCAL WALINZI WATATU WAUWAWA GEITA

WALINZI WATATU WAUWAWA GEITA

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni walinzi wa makampuni binafisi ya ulinzi katika mtaa wa Shilabela Kata ya Buhalala wilaya ya Geita Mkoani Humo wameuwawa na mtu ambae hajatambulika wakiwa wanatekeleza majuku yao ya ulinzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Ally Kitumbu amesema aliefanya mauaji hayo ni mtu mmoja alipofika eneo la tukio alitumia vipande vya ubao kisha kutekeleza mauaji hayo.

Amesema mpaka sasa jeshi la polisi linaendelea na msako Mkali Kwalengo la kuhakikisha wanamkamata mtu huyo aliehusika na mauaji hayo.

Mkuu wa wilaya Geita Wilson Shimo amekemea mauaji hayo na kuliagiza jeshi la polisi kuhakikisha uchunguzi unafanyika haraka ili mtu aliefanya mauaji hayo akamatwe haraka kwa lengo kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Shilabela wamesema matukio ya kuuwawa kwa walinzi yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kuiomba serikali kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo.

Previous articleMAAGIZO KWA WIZARA 5 UTUNZAJI MAZINGIRA 
Next articleWANAFUNZI WA VIJIJI VYA KITANGE, KITANGE ONE NA KIJIJI CHA USUNGU WILAYANI KILOSA WANATEMBEA UMBALI WA KILOMETA 36 KUFUATA SHULE.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here