Home BUSINESS BRELA YAPATA TUZO YA TPSF

BRELA YAPATA TUZO YA TPSF

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizotambuliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) katika siku ya TPSF, kutokana na mchango wake katika kukuza uwekezaji wa sekta binafsi nchini.

Hafla hiyo imefunguliwa rasmi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, tarehe 02 Novemba 2022. katika ukumbi wa The SuperDome Arena) Masaki, Jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Gofrey Nyaisa amekabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, BRELA ikiwa ni miongoni mwa Taasisi za Umma kadhaa zinazochangia katika ukuaji wa sekta binafsi na uchumi wa nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here