Home SPORTS SIMBA YAITUNGUA IHEFU 1-0 KWA MKAPA

SIMBA YAITUNGUA IHEFU 1-0 KWA MKAPA

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imebuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Simba ilipata bao la ushindi dakika ya 63 likifungwa na Pape Sakho bao lililodumu hadi dakika 90.

Kwa ushindi huo Simba imefikisha Pointi 21 nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 10 huku Azam FC wakikwea nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 23.

Mchezo mwingine Azam FC wameichakaza Mtibwa Sugar mabao 4_3 mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu Mkoa Morogoro. 

Ligi hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Kagera Sugar watawakaribisha Mabingwa watetezi Yanga ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 20 huku wakiwa wanacheza mechi nane.

Previous articleWANANCHI KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SERENGETI SAFARI MARATHON KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Next articleBARAZA LA WAFANYAKAZI BRELA LAPIGWA MSASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here