Home LOCAL RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MIKUTANO MBALIMBALI YA COP27, SHARM EL...

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MIKUTANO MBALIMBALI YA COP27, SHARM EL SHEIKH NCHINI MISRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika moja ya Mikutano ilioandaliwa na Benki ya Dunia kuhusu miradi mbalimbali ya Mazingira inayosaidia kupunguza hewa ukaa kwenye muendelezo wa COP 27 nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022. Mkutano huo ulioongozwa na Rais wa Benki ya Dunia David Malpass, pia umehudhuriwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyussi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Botswana Mhe. Mokgweetsi Masisi katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Watanzania waliofika kutembelea Banda la Maonesho la Tanzania lililopo ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wa Mazingira wa Tanzania mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Tanzania lililopo ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022.

Previous articleWAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI, NAIBU MAWAZIRI NA MAKATIBU WA KUU JIJINI DODOMA
Next articleASANTENI WATUMISHI WA AFYA KWA MLIVYOJITOA KATIKA AJALI YA NDEGE- DKT. MOLLEL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here