Home LOCAL ASANTENI WATUMISHI WA AFYA KWA MLIVYOJITOA KATIKA AJALI YA NDEGE- DKT. MOLLEL

ASANTENI WATUMISHI WA AFYA KWA MLIVYOJITOA KATIKA AJALI YA NDEGE- DKT. MOLLEL

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewashukuru Watumishi wa afya wote walijitokeza kuhudumia majeruhi katika ajali ya ndege iliyotokea katika Mkoa wa Kagera iliyotokea Novemba 6, 2022.

Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo leo Novemba 8, 2022 alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo kwa jitihada za Watumishi wa afya mpaka kufikia leo alibaki majeruhi mmoja tu.

Aidha, Dkt. Mollel amesisitiza Serikali itaendelea kugharamia majeruhi wote waliotokea katika ajali hiyo ya ndege mpaka watakapokuwa sawa kiafya.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya za Watanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu kama majengo ya dharura na kuwapa mafunzo Wataalamu ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia katika kuokoa hali ya majeruhi waliokuwa katika ajali ya ndege

Previous articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MIKUTANO MBALIMBALI YA COP27, SHARM EL SHEIKH NCHINI MISRI
Next articleMUUNDO MPYA IDARA YA TIBA KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA KWA KWA WAZEE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here