Home LOCAL JUNGU: BADO KUNA CHANGAMOTO YA KURATIBU MATUKIO YA VIONGOZI WA KITAIFA

JUNGU: BADO KUNA CHANGAMOTO YA KURATIBU MATUKIO YA VIONGOZI WA KITAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu yaliyoanza jana mkoani hapa..
Mkurugenzi  wa Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomea Jungu, akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu yaliyofanyika mkoani hapa jana na kufikia tamati leo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada.
Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKURUGENZI  wa Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomeo Jungu amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, sehemu ya Utawala  na Rasilimali Watu kushindwa kufuata Itifaki na Uratibu wa matukio ya viongozi wa kitaifa.

Jungu ameyasema hayo  jana mkoani Singida kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu.

Alisema  kuna baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu hawajui hata mavazi ya kuvaa pale kunapokuwa na viongozi wa kitaifa, huku wengine hawajui hata namna ya kula mbele ya viongozi wa kitaifa.

Aidha alisema mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki kwenye
matukio ya viongozi wa kitaifa kwa wakurugenzi yanatajwa kuwasaidia wakurugenzi hao kujua itifaki viongozi wa kitaifa wanapofika katika maeneo yao ya utendaji.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Ezavier Daud alisema  mafunzo hayo yatawasaidia kuondoa au kupunguza changamoto zinazojitokeza katika masuala ya itifaki kwa Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na Rasilimali watu.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba  alitoa wito kwa wakurugenzi hao na makatibu awala wasaidizi kuyatumia mafunazo haya kuwa suluhisho la makosa yanayojitokeza kwenye suala la itifaki.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo haya wamesema mafunzo hayo yatawasaidia
kujua kujua itifaki Kwenye matukio ya viongozi wa kitaifa wanapotembelea maeneo
yao.
 

Previous articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA KWENYE MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 50 YA UTUME NA HUDUMA YA KANISA LA WA ADVENTISTA WASABATO JIJINI DODOMA
Next articleRAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA KUFUNGUA MKUTANO WA MABALOZI WA TANZANIA UNAOFANYIKA ZANZIBAR TAREHE 19-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here