Home LOCAL WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YAITAKA BODI YA MPYA BARAZA LA TAIFA...

WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YAITAKA BODI YA MPYA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI KUTEKELEZA MAJUKUMU YENYE KULETA TIJA

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa Mhandisi Matiko Mturi akifafanua jambo wakari wa kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa bodi mpya ya baraza hilo pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete pamoja na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ludovicky Nduyiye(hawakopichan).

Sehemu ya wajumbe wa bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa wakiwa makini kufuatilia maelekezo na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete(hayuko pichani) wakati wa kikao hicho.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete akiwa makini kusikilia mijada mbalimbali iliyokuwa ikitolewa wa kikao hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa Dk.Fatma Mohamed (katikati) wakijadiliana jambo na wajumbe wengine baada ya kumalizika kwa kikao chao na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete(hayuko pichani)

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa Mhandisi Matiko Mturi(kulia) akifurahia jambo pamoja na wajumbe wengine wa bodi ya baraza hilo walipokuwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete(hayuko kwenye picha).

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete(wa pili kulia) akisikiliza kwa makini majadiliano ya baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya baraza hilo baada ya kumalizika kwa kikao.

Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa wakijadiliana baada ya kumalizika kwa kikao kati yao na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa Dk. Fatma Mohamed  akizungumza jambo kwenye kikao hicho.

Naibu Waziri wa Ujenzi la Taifa Atupele Mwakibete (kulia) akifurahia jambo na baadhi ya wajumbe wa bodi ya baraza hilo.

Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Ujenzi la Taifa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele  Mwakibete(hayuko pichani) leo Oktoba 20 mwaka 2022 .(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE)

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa leo Oktoba 20,2022 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na bodi hiyo.Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk.Fatma Moamed  na wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa Mhandisi Matiko Mturi.

Na: Said Mwishehe,Michuzi TV

WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi imeitaka Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Ujenzi kutekeleza majukumu manne yatakayoleta tija katika sekta hiyo ikiwemo, kuwepo kwa kanuni ya majenzi,sheria ya majenzi,miongozo ya majenzi na kuifanya tasnia hiyo iheshimike.

Akizungumza Dar es Salaam leo Oktoba 20 mwaka wakati wa uzinduzi wa bodi ya baraza hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete ameeleza kwamba Serikali inategemea bodi hiyo kufanya  kazi yake kwa miaka mitatu na kutekeleza majumu waliyopewa.

Amefafanua anazijua changamoto za taasisi hiyo ikiwemo kutopata fedha za maendeleo kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za maendeleo, lakini anaamini kuwepo kwa bodi hiyo yenye wataalamu wa kutosha kila kitu kitakwenda sawa ndani ya sekta hiyo.

Ameongeza anaamini  bodi hiyo ina uzoefu wa kutosha kwa sababu kila mjumbe ametoka katika taasisi yake hivyo wakijumuika pamoja watafanya mambo mazuri yenye kuleta tija katika taasisi hiyo.

Pamoja na hayo Naibu Waziri Mwakibete ameishauri bodi hiyo kuhakikisha wanaondoa changamoto ya  wataalamu wa ujenzi wa barabara kutokuwa na tathimini ya uhakika katika miradi yao.

“Bodi hakikisheni tathimini zinazopelekwa serikalini zinakuwa ni za uhakika na zenye kumaliza mradi uliopo kwani kazi yenu ni  kuleta mabadiliko makubwa katika taasisi,”amesema na kuongeza Baraza hilo lina umuhimu kwa Taifa kwa sababu linachangia asilimia 14 ya pato la Taifa.

Kwa upande wake Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ludovick Nduhiye ameongeza kuwa wanategemea mabadiliko mazuri ndani ya taasisi hiyo kutokana na ubora wa bodi iliyopo huki akiitaka bodi hiyo kuhakikisha inatekeleza maagizo waliyopewa ili iweze kuleta tija ndani ya taasisi hiyo na Taifa.

 

Wakati Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk. Fatma Mohamed ametumia nafasi hiyo kuihakikishia Serikali kuwa bodi hiyo itafanyia kazi kwa weledi yale yote waliyoagizwa ili kubadilisha sura ya taasisi hiyo na Taifa liongeze  uchumi.

Dk Mohamed amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitatu watahakikisha wanafanya yenye kuleta tija na mafanikio makubwa kwenye sekta ya ujenzi nchini.

Mwisho

Previous articleTANZANIA YAPIGA HATUA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA
Next articleWORLD VISION TANZANIA  YATOA VIFAA VYENYE THAMANI MILIONI 152 KWA SHULE ZA MSINGI YA UYUI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here