Home LOCAL WADAU WA MAENDELEO WAHIMIZWA KUCHANGIA VIFAA VYA MISAADA YA KIBINADAMU WAKATI WA...

WADAU WA MAENDELEO WAHIMIZWA KUCHANGIA VIFAA VYA MISAADA YA KIBINADAMU WAKATI WA MAAFA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati alipotembellea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada  wa kibinadamu wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.

Afisa Ugavi Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro Bwa. Claude Kilala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga alipotembelea ghala hilo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (aliyeinama) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu (kulia)

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkoa huo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na: Mwandishi wetu- Kilimanjaro.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuchangia vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa.

Mhe. Ummy aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa Kanda ya Kaskazini  lililopo maeneo ya Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Alisema uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.

“Nitoe wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngaji ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,” alihimiza Mhe. Ummy.

Pia Mhe. Ummy alisisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika maeneo yenye maafa.

Aidha aliupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea katika hali yao ya awali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Afisa Mifugo katika Mkoa huo  Bwa. James Shao alisema ghala la Kanda ya Kasikazini linahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

MWISHO.

Previous articleTASAF HALMASHAURI YA WILAYA SONGEA YAENDELEA KUMWAGA UPENDO KWA JAMII,YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 395 KUTEKELEZA MIRADI 6 JIMBO LA PERAMIHO
Next articleSERIKALI YAOMBA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here