Home LOCAL TASAF HALMASHAURI YA WILAYA SONGEA YAENDELEA KUMWAGA UPENDO KWA JAMII,YATOA ZAIDI YA...

TASAF HALMASHAURI YA WILAYA SONGEA YAENDELEA KUMWAGA UPENDO KWA JAMII,YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 395 KUTEKELEZA MIRADI 6 JIMBO LA PERAMIHO

Katibu tawala Wilaya ya Songea Pendo Daniel, akizungumza wakati wa mkutano wa utambulishaji fedha za miradi 6 yenye thamani ya shilingi milioni 395 zilizotolewa mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF Katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo Halmashauri ya wilaya Songea.

Na: Muhidin Amri, Songea.

SERIKALI kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF), imetoa zaidi ya shilingi milioni 395 kutekeleza miradi 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo  katika Halmashauri ya wilaya Songea.

Akizungumza kwenye mkutano huo mbele ya uongozi wa Halmashauri  pamoja na Wananchi, alisema kukamilika kwa miradi hiyo italeta tija kwao  kwani itawawezesha wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini na jamii kufanya biashara za uhakika  na  hivyo ni jukumu lao kushiriki hatua zote za ujenzi wa miradi hiyo

Alisema,kati ya Fedha  hizo, kijiji cha Parangu  kimepokea shilingi milioni 225 za ujenzi wa miradi mitatu ambapo ni standi, uwekaji wa vigaya pamoja na kujenga matundu manne ya vyoo na uzio.

Aidha,kijiji cha Mdunduwalo kimepokea shilingi milioni 170 za ujenzi wa miradi mitatu ujenzi wa nyumba ya madaktari wawili, matundu sita ya vyoo pamoja na uchimbaji wa kisima kirefu cha maji.

“Ni matumaini yangu miradi hii itakuza uchumi wa kaya pamoja na kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja pia kujengwa kwa miradi hii 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo  itaongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii”alisema  Daniel.

Hata hivyo, amewasisitiza viongozi wa vijiji pamoja na kamati za ujenzi wa miradi hiyo kushirikiana na wananchi katika kutekeleza ujenzi kwani asilimia 10 ya ujenzi itatolewa na wananchi katika kufanikisha kukamlikia kwa miradi yote

Kwa upande wake Mwenyekeiti wa Halmashauri hiyo Menasi Komba,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kwa uamuzi wake wa kutoa fedha hizo za miradi ambazo zitatumika kujenga miradi hiyo  na kuwaomba wananchi wailinde mradi hiyo nakushiriki hatua zote za ujenzi.

“Wale wote watakaobainika kuiba zivifaa vya ujenzi kwenye miradi hii hatua zitachukuliwa haraka, pia niwaombe wajumbe na wanakamati wa miradi wa vijiji vyote viwili msishawishike hizi fedha zimeletwa kwa malengo ya kukuza uchumu wa kaya zetu”alisema Komba.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake Nicodemus Nyoni mkazi wa kijiji cha Parangu, amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Jenista  Mhagama kwa kuweza kupeleka fedha za miradi wa ujenzi wa stendi ambapo itakapokamilika itawasaidia kujipatia kipato na kuwa na uhakika wa kupata huduma mbalimbali.

Previous articleKUTOKA MAGAZETINI ASUBUHI YA LEO JUMATANO OKTOBA 12-2022
Next articleWADAU WA MAENDELEO WAHIMIZWA KUCHANGIA VIFAA VYA MISAADA YA KIBINADAMU WAKATI WA MAAFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here