Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano (TALGWU) Shani Kibwasali akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9,2022 katika Ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAM
CHAMA Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeiangukia Serikali kuliangalia upya suala la tozo kwakupitia upya sheria ya tozo za miamala ya kibenki ili kuepuka malipo mara mbili wanayokatwa kutokana na kuwa na mishahara midogo na kushindwa kukidhi mahitaji ya familia zao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano (TALGWU) Shani Kibwasali amesema kuwa licha ya kuwepo kwa Suala la tozo lakini Chama hicho kimekuwa kikishirikiana na vyama vingine vya wafanyakazi kulishughulikia chini ya umoja wa vyama vya wafanyakazi TUCTA ambapo amesema kuwa serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshapokea mapendekezo ya vyama hivyo na kuahidi kulishughulikia.
Ameongeza kuwa watumishi wa umma kila mwezi wanalipa kodi kwa kukatwa katika mishahara yao. Lakini sasa kuanza kutekelezwa kwa sheria hii ya tozo inamfanya mtumishi wa umma kutozwa zaidi ya mara mbili katika pato moja kwa mwezi,” amesema Shani Kibwasali
“Niwaombe wanachama wetu tuendelee kuwa watulivu tukisubiri utekelezaji wake kwani tunaamini serikali yetu ni sikivu na suala hili litapatiwa ufumbuzi haraka,’.Amesema Kibwasali.