Home BUSINESS TRA YAPIGA MSASA WANACHAMA WA TWCC KUHUSU SHERIA YA FEDHA YA MWAKA...

TRA YAPIGA MSASA WANACHAMA WA TWCC KUHUSU SHERIA YA FEDHA YA MWAKA 2022/2023

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumza katika mkutano wa Wanawake wafanyabiashara (Women in Business Breakfast Meeting) uliofanyika leo Septemba 10,2022 katika ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla (kushoto) akizumza katika mkutano huo juu ya fursa mbalimbali zilizopo kwa wanawake ikiwemo mikopo inayotolewa na Halmashauri zote Nchini.

Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo kabla ya kutoa mada iliyolenga kutoa Elimu ya Kodi na ufafanuzi juu ya Sheria ya fedha ya mwaka 2022/2023.

Afisa Mkuu wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Deodatus Kabuteni akitoa Elimu ya Kodi na ufafanuzi juu ya Sheria ya fedha ya mwaka 2022/2023 kwa wanawake wafanyabiashara wanaoshiriki Mkutano maalum wa mwezi ulioandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Jijini Dar es Salaam.

Muhamasishaji wa masuala ya Biashara Charles Nduku (Mr. Brand) akizungumza katika mkutano huo.

Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji na Usimamizi wa Rasilimali Tanzania (UTT) Esther Kahabi akitoa mada kwa wanawake wafanyabiashara waliohudhuria  mkutano wa Wanawake wafanyabiashara (Women in Business Breakfast Meeting) uliofanyika leo Septemba 10,2022 katika ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya washiriki walioudhuria Mkutano huo.

Afisa Wanachama wa TWCC Cresesia Mbunda akizungumza kwenye mkutano.

Mratibu wa TWCC SACCOS Nelson Clevery kutoka (TWCC) akizungumza na washiriki wa mkutano huo juu ya fursa ya mikopo mbalimbali inayopatikana katika SACCOS hiyo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).

NA: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kimetoa Elimu ya Kodi kwa wanachama wake pamoja na Ufafanuzi juu ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2022/2023 katika Mkutano wao wa Mwezi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum katika Mkutano wa Wanawake Wafanyabiashara (Women in Business Breakfast Meeting) uliofanyika leo Septemba 10,2022 katika Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma hamza amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha wananchama zaidi ya 200 na wengine zaidi ya 300 wamefuatilia kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa Chama hicho kimekuwa na utaratibu mzuri wa kukutana kila mwezi ambapo katika mkutano huo wameweza kutoa Elimu mbalimbali kwa wanachama wao ikiwemo Elimu ya Kodi na Ufafanuzi juu ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2022/2022 iliyotolewa na Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Lengo la Mkutano huu ni kwaajili ya kuwaleta pamoja wanancha wetu kwa lengo la kufahamiana na kupeana taarifa pamoja na kutafuta masoko lakini Mada kubwa ni kuhusu Sheria ya fedha ya mwaka 2022/2023 pamoja na Elimu ya Kodi ili wanachama wetu waweze kufahamu Sheria hiyo na Masuala ya Kodi kwa Ujumla”

“Tunataka Wanachama wetu wapate hii Elimu vizuri waitambue ili wanapofanya Biashara zao wawe na uelewa wa Sheria hii ili iwasaidie pale watakapokuwa wanalipa Kodi” amesema Mwajuma.

Aidha amesema kuwa katika mkutano huo pia walikuwepo wadau kutoka katika Taasisi za Serikali wakiwemo Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji na Usimamizi wa Rasilimali Tanzania (UTT) waliokuwa wakitoa Elimu juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba zitakazowasaidia kwenye shuguli zao na familia kwa ujumla.

“Kama tunavyofahamu wafanyabiasahara wana changamoto nyingi ndio mana tunawahimiza kujiwekea akiba UTT kwaajili ya biashara zao lakini kwaajili ya kusomesha watoto wakati wao wakiendelea na Biaashara basi kuwepo na sehemu ambayo watakuwa wamewekeza na kupata gawio” amesema mwajuma.

Pia katika mkutano huo kulikuwepo na wataalamu wa Sheria waliotoa mada juu ya msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara hao kwa lengo la kutoa uelewa na kuwajengea uwezo kufahamu namna wanavyoweza kuendesha biashara zao kisheria na kujua njia gani za kufuata endapo watapata changamoto za kisheria katika Bishara zao.

Katika hatua nyinge Mwajuma amezungumzia ziara ya Biashara na Uwekezaji inayotajarajia kufanyika Octomba 11 hadi 19, 2022 yenye lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya viwanda pamoja na maonesho ya Kilimo, Mashine na zana za Kilimo.

Amesema kuwa uwepo wa ziara hiyo ni fursa kubwa kwa wafanyabiasha hao kuongeza wigo wa kujifunza na kuongeza uelewa juu ya masula mbalimbali za kibiashara, usindikaji wa vyakula na Kilimo kwa ujumla.

“Maonesho ni muhimu sana kutokana na kuwa na sekta tofauti kama urembo na sekta ya vipodozi, pia yapo yanayohusiana na vyakula na usindikaji na utunzaji wa vyakula hivyo wale ambao wapo kwenye sekta hii haya maonesho yanawafaa, kutakuwa na Bidhaa za samani pamoja na kutembelea viwanda” amesema.

Awali katika mkutano huo Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla amezungumzia uwepo wa fursa ya mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri inayopatikana kwenye halmashauri zote nchini ambapo amesema kuwa wanawake ni sehemu ya makundi yaliyotengewa fedha hizo hivyo kuwahimiza wananchama hao kuhakikisha wanapata mikopo hiyo ili kuongeza mitaji katika biashara zao.

Previous articleTALGWU YAIANGUKIA SERIKALI SAKATA LA TOZO
Next articleUTEKELEZAJI WA DHANA YA AFYA MOJA WAANZA KWA KASI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here