Home LOCAL TALGWU YAIANGUKIA SERIKALI SAKATA LA TOZO

TALGWU YAIANGUKIA SERIKALI SAKATA LA TOZO

Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano (TALGWU) Shani Kibwasali akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9,2022 katika Ofisi za chama hicho  jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeiangukia Serikali kuliangalia upya suala la tozo kwakupitia upya  sheria  ya tozo za miamala ya kibenki ili kuepuka malipo mara mbili wanayokatwa kutokana na kuwa na mishahara midogo na kushindwa kukidhi mahitaji ya familia zao.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano (TALGWU) Shani Kibwasali amesema kuwa licha ya kuwepo kwa Suala la tozo lakini Chama hicho kimekuwa kikishirikiana na vyama vingine vya wafanyakazi  kulishughulikia chini ya umoja wa vyama vya wafanyakazi TUCTA ambapo amesema kuwa  serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshapokea mapendekezo ya vyama hivyo na kuahidi kulishughulikia.

Ameongeza kuwa watumishi wa umma kila mwezi wanalipa kodi kwa kukatwa katika mishahara yao. Lakini sasa kuanza kutekelezwa kwa sheria hii ya tozo inamfanya mtumishi wa umma kutozwa zaidi ya mara mbili katika pato moja kwa mwezi,” amesema Shani Kibwasali

“Niwaombe wanachama wetu tuendelee kuwa watulivu tukisubiri utekelezaji wake kwani tunaamini serikali yetu ni sikivu na suala hili litapatiwa ufumbuzi haraka,’.Amesema Kibwasali.

 

 

 

 

Previous articleTARURA ILALA YATENGA BAJETI SHILINGI BIL 25.2 ZA BARABARA
Next articleTRA YAPIGA MSASA WANACHAMA WA TWCC KUHUSU SHERIA YA FEDHA YA MWAKA 2022/2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here