Home ENTERTAINMENTS KAMPUNI YA TIGO, BOOMPLAY KUNUFAISHA WASANII WA MUZIKI NCHINI

KAMPUNI YA TIGO, BOOMPLAY KUNUFAISHA WASANII WA MUZIKI NCHINI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Septemba 7,2022 Jijini Dar es Salaam

Meneja  Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (katikati) akizungumza katika mkutano huo. (Kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga, na (kushoto), 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mario (katikati) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Leo Septemba 7,2022 Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

WASANII wa muziki nchini wameendelea kupata fursa za kutangaza na kuuza kazi zao za muziki baada ya kampuni ya huduma za simu ya Tigo na kampuni ya muziki mtandaoni Boomplay kuungana kwa ajili ya kuwapa fursa wapenzi na mashabiki wa muziki kusikiliza mtandaoni.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza fursa hiyo iliyofanyika leo Septemba 7,2022 Jijini Dar es Salaam, mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Mario amesema kuwa huduma hiyo mpya ya kusikiliza muziki kupitia mtandao kwenye ‘App’ ya Boomplay itazidi kuwatangaza wasanii na kuwaingizia kipato kutokana na kazi zao kusikilizwa.

Amesema kupitia kampeni mpya ya Tigo ya ‘Wakishua; mashabiki wa muziki watapata fursa kupakua na kusikiliza muziki wa wasanini mbalimbali.

“Binafsi nawashukuru sana Tigo na Boomplay kwa kuja na huduma hii ambayo ni fursa mpya kwa wasanii kuingiza kipato na kujitangaza Duniani kote”

Kwa upande wake, Meneja  Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli alisema  mpaka sasa kuna watu milioni 70 Duniani kote anaotumia Boomplay hivyo kuwapo kwa huduma hiyo kutatoa fursa kwa wasanii lakini pia mashabiki kusikiliza nyimbo wazitakazo mtandaoni.

“Muungano huu na Tigo utatoa fursa kwa watumiaji wa huduma za kampuni hii ya simu hapa Tanzania kuwasikiliza wanamuziki wao pendwa,” amesema, Natasha.

Aidha, kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga, aliema mtandao wa Tigo umekuwa ukisaidia tasnia ya muziki kwa kutoa fursa kwa wasanii kuungana na mashabiki zao.

“Kupitia kampeni yetu ya ‘Wakishua’ mashabiki wetu watapata hii huduma kwa gharama ile ile, lengo ni kuhakikisha Tigo inawasogeza wasanii karibu na mashabiki wao,” amesma Mpinga.

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi Leo Septemba 7,2022 Jijini Dar es salaam ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wamehudhuria.

Previous articleINTERNATIONAL NEWSPAPERS FOR SEPTEMBER 7-2022
Next articleSHERIA YA KULINDA DATA BINAFSI KUJADILIWA BUNGENI MWEZI HUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here