Afisa TEHAMA toka TAMISEMI Godfrey Isinika akitoa mafunzo kwa maafisa Habari.
Baadhi ya maafisa Habari wakiwa katika majadiliano kuhusiana na kile walichojifunz
Na: Devota Mwachang’a, Mwanza
Maafisa habari wa Halmashauri nchini wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa sahihi za maendeleo kwenye halmashauri zao ikiwemo miradi ya kuimarisha utekelezaji wa elimu bora nchini.
Ushauri huo umetolea na Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) toka TAMISEMI Godfrey Isinika akielezea umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kwa wadau wa Habari nchini kusambaza taarifa sahihi na zenye tija kwa sekta ya elimu.
“Yatumieni makundi yenu ya mitandao ya kijamii (social media) kutuma link zinazoambatana na taarifa fupi itakayowezesha wasomaji kutembelea moja kwa moja kwenye kurasa za taasisi badala ya kutuma picha tu,” amesema Isinika.
Maafisa Habari toka mikoa ya Mara, Simiyu na Singida wanakutana Mwanza katika mafunzo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Shirika na Cambridge Education Tanzania kupitia Mradi wa serikali wa Shule Bora unaofadhiriwa na Shirika la maendeleo la Uingereza( UKaid). Mafunzo haya nimoja wapo ya mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa taarifa, uandishi na usambazaji wa habari za elimu bora katika mikoa tisa ya tanzania.