Home LOCAL CAMBRIDGE EDUCATION TANZANIA YAWAKETISHA MAAFISA HABARI WA HALMASHAURI KUWAJENGEA UWEZO JIJINI MWANZA

CAMBRIDGE EDUCATION TANZANIA YAWAKETISHA MAAFISA HABARI WA HALMASHAURI KUWAJENGEA UWEZO JIJINI MWANZA

Afisa TEHAMA toka TAMISEMI Godfrey Isinika akitoa mafunzo kwa maafisa Habari.

Baadhi ya maafisa Habari wakiwa katika majadiliano kuhusiana na kile walichojifunz

Na: Devota Mwachang’a, Mwanza

Maafisa habari wa Halmashauri nchini wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa sahihi za maendeleo kwenye halmashauri zao ikiwemo miradi ya kuimarisha utekelezaji wa elimu bora nchini.

Ushauri huo umetolea na Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) toka TAMISEMI Godfrey Isinika akielezea umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kwa wadau wa Habari nchini kusambaza taarifa sahihi na zenye tija kwa sekta ya elimu.

“Yatumieni makundi yenu ya mitandao ya kijamii (social media) kutuma link zinazoambatana na taarifa fupi itakayowezesha wasomaji kutembelea moja kwa moja kwenye kurasa za taasisi badala ya kutuma picha tu,” amesema Isinika.

Maafisa Habari toka mikoa ya Mara, Simiyu na Singida wanakutana Mwanza katika mafunzo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Shirika na Cambridge Education Tanzania kupitia Mradi wa serikali wa Shule Bora unaofadhiriwa na Shirika la maendeleo la Uingereza( UKaid). Mafunzo haya nimoja wapo ya mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa taarifa, uandishi na usambazaji wa habari za elimu bora katika mikoa tisa ya tanzania.

Previous articleKANAL HEMED AZINDUA TIKETI ZA KIDUKU MTWARA
Next articleTANZANIA IS CONGRATULATED FOR BEING AN ACTIVE MEMBER OF THE AFRICAN UNION
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here