Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MASANJA: WAVAMIZI WA HIFADHI YA MSITU WA BONDO WATAKIWA KUONDOKA...

NAIBU WAZIRI MASANJA: WAVAMIZI WA HIFADHI YA MSITU WA BONDO WATAKIWA KUONDOKA IFIKAPO DESEMBA 30

Wananchi waliovmia Hifadhi ya Msitu wa Bondo wametakiwa kuondoka ndani ya hifadhi hiyo ifikapo Desemba 30,2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi Mhe. Omar Mohamed Kigua bungeni jijini Dodoma leo Septemba 19,2022.

“Kwa nyakati tofauti hifadhi hii imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu zikiwemo kilimo,makazi na kuchungia mifugo” Mhe. Masanja amefafanua.

Amesema Serikali imeweka matangazo ya kuwataka wananchi wote kuondoka ndani ya hifadhi hiyo.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali misitu nchini.

Hifadhi ya Msitu wa Bondo, ipo katika Kijiji cha Mswaki,Kata ya Msanja Wilayani Kilindi Mkoani Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here