Home LOCAL TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA TATU MWAKA WA MASOMO 2022/2023

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA TATU MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Na: Hughes Dugilo, Dar es Salaam.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua Dirisha  la Udahili kwa Awamu ya Tatu kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023.

Akizungumza kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Septemba 19,2022 Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Charles Kihampa amesema kuwa Dirisha hilo limefunguliwa rasmi kuanzia leo Septemba 19 hadi 25, 2022 na kwamba Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali watumie vizuri fursa hio kwa kutuma kwa usahihi maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

“Tume inaelekekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa shahada ya kwanza kuendelea kutangaza Programu ambazo bado zina nafasi. Aidha, waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya Tatu kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyo katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)” amesema Prof. Kihampa.

Pia Prof. Kihampa amewakumbusha waombaji wote wa udahili wa Shahada ya Kwanza  kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika Chuo kimoja  yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika, na kwamba kwa wale ambao watapata changamoto ya kujithibitisha, Vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

Aidha TCU inawaasa wananchi kujihepusha na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu.

Awali katika taarifa hiyo TCU imeufahamisha Umma na wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa Awamu ya Pili ya Udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 imekamilika, na kwamba majina yawaombaji waliodahiliwa katika Awamu ya pili yanatangazwa na vyuo husika.

Aidha waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza na ya Pili wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 19 hadi 25 Septemba, 2022 kwa kutumia nambamalum ya siri iliyotumwa kuomba udahili.

“Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo vinavyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika”

Previous articleNAIBU WAZIRI MASANJA: WAVAMIZI WA HIFADHI YA MSITU WA BONDO WATAKIWA KUONDOKA IFIKAPO DESEMBA 30
Next articleMWENEKITI TEF ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA MALIKIA ELIZABETH II
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here