Home LOCAL ASKOFU MKUU WA KANISA ANGLIKANA ATOA WITO TANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA KUEPUKA UKAME

ASKOFU MKUU WA KANISA ANGLIKANA ATOA WITO TANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA KUEPUKA UKAME

Na: Maiko Luoga Tanga.

Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Maimbo Mndolwa amewashauri Wakristo na Watanzania nchini kutunza mazingira ikiwemo kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kupunguza hali ya ukame inayoweza kuikumba nchi na Dunia kwa ujumla.

Ametoa ushauri huo agosti 24, 2022 wakati akiongoza Misa takatifu ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Kanisa Anglikana Kivindo lililopo Muheza Dayosisi ya Tanga.

“Tunaona hili anga lilivyo wenzetu wanasayansi walikisia kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo huenda kukawa na ongezeko la joto kwa asilimia 1.5 lakini Sasa wanasema hali hiyo naweza kuongezeka kwa asilimia 2.5 ongezeko la asilimia moja zaidi”

“Hali hii maana yake vyanzo vingi vya maji vitakauka, mazingira yetu yatakuwa na ukame mkubwa, tuliombe Kanisa na Watanzania wote tunapoona mvua inanyesha tuitumie kupanda miti, maji kidogo tunayopata tuyatumie vizuri hii ni rasilimali kubwa”

“Kuna kawaida ya kufikiri maji sio rasilimali kwahiyo yanachezewa sana, pia tuna kawaida ya kukata miti ovyo miaka ya nyuma maeneo yetu ya nchi yalitawaliwa na misitu ya kutosha tofauti na ilivyo sasa tumejimaliza wenyewe tuwaombe sana kama Kanisa maeneo yetu yaliyo wazi tupande miti ili kudhibiti hali hii hapo baadae” ameeleza Askofu Maimbo Mndolwa.

Aidha Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania amewasisitiza Watanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ili kukamilisha lengo la Serikali la kupata hesabu ya watanzania kupitia Sensa ya watu na makazi inayoendelea kote nchini.

“Niwaombe watanzania tuendelee kushiriki zoezi hili la Sensa ya watu na makazi linaloendelea katika maeneo yetu, jambo hili ni muhimu sana kwetu ili kuidhihirishia Serikali kuwa Watanzania tupo wengi ili huduma zitufikie kulingana na idadi yetu.

Baadhi ya Waumini walioshiriki Misa hiyo wamekiri kupokea ushauri wa Askofu Mndolwa na kuahidi kufanyia kazi ili mazingira yaendelee kubaki salama huku wakiahidi kushiriki kwa ukamilifu zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Previous articleTCU YATANGAZA KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA MWAKA WA MASOMO 2022/2023
Next articleSENSA YA WATU NA MAKAZI INAENDELEA VIZURI,IMEVUKA MATARAJIO, ITAKUWA KWA SIKU SABA – ANNE MAKINDA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here