Home SPORTS KMC YAINGIA KAMBINI KUJINOA KWA MICHEZO YA LIGI KUU

KMC YAINGIA KAMBINI KUJINOA KWA MICHEZO YA LIGI KUU

Mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, kikosi cha KMC FC kimendelea na maandalizi ya kujiweka sawa katika michezo ya Ligi kuu ya NBC Soka Tanzaia bara dhidi  itakayoendelea Septemba saba mwaka huu.

KMC FC ambayo ilikuwa Jijini Arusha kwenye michezo miwili ya ugenini, ilirejea siku ya Jumatatu na kutoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ambapo jana Jumanne Agosti 23 jioni waliingia kambini na kuanza kwa program ya timu na leo hii asubuhi kuendelea na mazoezi ya kawaida ya uwanjani.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana katika kipindi hiki cha mapumziko kitakuwa na programu mbalimbali ikiwemo kucheza mechi za kirafiki ambapo kesho Agosti 25 itakuwa ugenini dhidi ya As Arta Solar 7 kutoka Nchini Djibout mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es Salaam.

Mbali na mchezo huo, KMC FC pia itakuwa na mechi nyingine za kirafiki kulingana na mipango ya Kocha Mkuu Hitimana ikiwa ni katika mpango wa kufanya maboresho kutokana na kile alichokiona katika michezo miwili ya awali ya Ligi kuu ya NBC ambayo ni dhidi ya Polisi Tanzania pamoja na Coast Union iliyopigwa katia uwanja wa Shekh Amri Abeid.

“Tumetoka kwenye mechi ngumu za ugenini, nakupata matokeo ambayo hayakuwa rafiki sana kama ambavyo malengo ya Timu ilikuwa imejiwekea ya kupata alama sita lakini tukapata alama moja na magoli mawili, wachezaji wetu walicheza vizuri hilo ni jambo kubwa.

Kwa kipindi hiki ambacho tupo kwenye mapumziko ya kupisha michuano ya kombe la Chani dhidi ya Uganda, tunahitaji mechi nyingi za kirafiki kadiri ambavyo tutazipata, na tayari tumeshapata mechi moja ambayo tutacheza kesho lengo ni kufanya maboresho ambayo yataiwezesha Timu kufanya vizuri zaidi katika michezo inayokuja.

KMC FC imecheza mechi mbili za Ligi Kuu ambazo ni dhidi ya Coast Union uliomalizika kwa kupoteza na mwingine ni Polisi Tanzania uliomalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili.

Previous articleVODACOM “BRING YOUR CHILD TO WORK” YAWAJENGEA WATOTO UFAHAMU WA MASOMO YA SAYANSI
Next articleWAZIRI MKUU AUNGANA NA MAMIA KUMUAGA MREMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here