Home KIDSNEWS VODACOM “BRING YOUR CHILD TO WORK” YAWAJENGEA WATOTO UFAHAMU WA MASOMO YA...

VODACOM “BRING YOUR CHILD TO WORK” YAWAJENGEA WATOTO UFAHAMU WA MASOMO YA SAYANSI

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kulia) akizungumza na watoto wa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work” inayoendana na huduma za Vodacom, pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku. Kushoto ni mtoa mafunzo hayo, Dkt. Isaya Ipyana kutoka Taasisi ya Project Inspire.
Kampuni inayoongoza kutoa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania imeendelea na mpango wake wa kila mwaka wa  kuwezesha watoto wa wafanyakazi wao kuwa na uwezo mzuri wa ufahamu wa masomo ya sayansi na pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis alisema ” Kupitia mpango huu Vodacom imewaandalia watoto wetu mafunzo ya masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work” inayoendana na huduma za zetu”. 
Alisema Vodacom ni kampuni ya mawasiliano na teknolojia hivyo wameonelea watoto wakutane pamoja kujua namna gani sayansi na teknolojia inavyofanya kazi ili hapo baadae nao waweze kupenda sekta hii. Mpango huu ni endelevu na ni mwaka wa tano sasa tokea uanzishwe, “Japokuwa tuliusitisha kutokana na janga la uviko 19, na tukawa tunafanya kupitia online.”
Pia mpango huu hauishii tu kuwaleta pamoja watoto bali waliwaandalia program maalum wanapokuwa majumbani ili wasisahau mafunzo waliyopata. 
“Vodacom kwenye  malengo yetu tunawezesha pia wanafunzi wasichana wa shule za sekondari kote nchini kupitia mpango wa “Code like a girl” ili kuwapa uelewa wa Tehama kwa kubuni tovuti na kupata uwezo wa teknolojia.”
Previous articleSENSA YA WATU NA MAKAZI INAENDELEA VIZURI,IMEVUKA MATARAJIO, ITAKUWA KWA SIKU SABA – ANNE MAKINDA
Next articleKMC YAINGIA KAMBINI KUJINOA KWA MICHEZO YA LIGI KUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here