Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kulia) akizungumza na watoto wa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work” inayoendana na huduma za Vodacom, pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku. Kushoto ni mtoa mafunzo hayo, Dkt. Isaya Ipyana kutoka Taasisi ya Project Inspire.
Kampuni inayoongoza kutoa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania imeendelea na mpango wake wa kila mwaka wa kuwezesha watoto wa wafanyakazi wao kuwa na uwezo mzuri wa ufahamu wa masomo ya sayansi na pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis alisema ” Kupitia mpango huu Vodacom imewaandalia watoto wetu mafunzo ya masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work” inayoendana na huduma za zetu”.
Alisema Vodacom ni kampuni ya mawasiliano na teknolojia hivyo wameonelea watoto wakutane pamoja kujua namna gani sayansi na teknolojia inavyofanya kazi ili hapo baadae nao waweze kupenda sekta hii. Mpango huu ni endelevu na ni mwaka wa tano sasa tokea uanzishwe, “Japokuwa tuliusitisha kutokana na janga la uviko 19, na tukawa tunafanya kupitia online.”
Pia mpango huu hauishii tu kuwaleta pamoja watoto bali waliwaandalia program maalum wanapokuwa majumbani ili wasisahau mafunzo waliyopata.
“Vodacom kwenye malengo yetu tunawezesha pia wanafunzi wasichana wa shule za sekondari kote nchini kupitia mpango wa “Code like a girl” ili kuwapa uelewa wa Tehama kwa kubuni tovuti na kupata uwezo wa teknolojia.”