Home INTERNATIONAL WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA FINLAND

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA FINLAND

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Pekka Haavisto pembezoni mwa Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika tarehe 13 hadi 15 Juni 2022 jijini Helsinki, Finland.

Serikali ya Tanzania na Finland zinashirikiana katika masuala ya ubunifu wa kutengeneza ajira, usimamizi wa fedha kwa taasisi za umma, kujenga uwezo kwenye masuala ya kodi pamoja na utawala bora.
Maeneo mengine ya kipaumbele katika ushirikiano huo ni pamoja na elimu,kuinua ubia kati serikali na sekta binafsi, kuhamasisha uwekezaji, umarishaji wa demokrasia na utawala wa sheria na kukuza biashara.

 

Balozi wa Tanzania nchini Finland mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Grace Alfred Olutu na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo.



Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Pekka Haavisto akieleza utayari wa Serikali ya Finland katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya Serikali yake na Tanzania.

 

Ujumbe ulioambatana na Mhe. Haavisto ukifuatilia mazungumzo.
Previous articleBALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA ATEMBELEA OFISI YA WAZIRI MKUU
Next articleMEYA KUMBILAMOTO ATAKA FAHARI WAUNGWE MKONO KUKOMESHA UKATILI KWA WATOTO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here