Home LOCAL WANANCHI 8,644 KIJIJI CHA KASEME WAONDOKANA NA KERO YA MAJI

WANANCHI 8,644 KIJIJI CHA KASEME WAONDOKANA NA KERO YA MAJI
Na: Costantine James, Geita

Wananchi wa kijiji cha Kaseme kata ya Kaseme wilayani Geita mkoani Geita wameishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji katika eneo lao.

Wananchi hao wamesema zaidi ya miaka 10 wamekuwa na kero ya ukosefu wa maji safi na salama na sasa serikali imetatua changamoto hiyo kwa kukamilisha mradi wa maji chini ya usimamizi wa ofisi ya RUWASA mkoa , wilaya pamoja na wananchi wa kijiji cha Kaseme.

Wamesema kabla ya kukamilika kwa mradi huo wananchi walikua wanapata shida ya kufata maji umbali mrefu na  walikuwa waanachota maji mtoni  maji ambayo sio safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

 Wananchi hao wamesema uwepo wa mradi huo sasa utawasaidia kupata maji safi na salama kwa kalibu zaidi hali itakayowasaidia kuepukana mlipuko wa magojwa uliokuwa unasababishwa na matumizi ya maji ambayo sio safi na salama.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa amesema mradi huo umekamilika  kwa asilimia 100% na tayari wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa urahisi zaidi.

Mhandisi Sande amesema mradi huo utahudumia wananchi 8,644 wakazi wa kijiji cha kaseme kwakupata maji safi na salama na utawezesha kupunguza muda kwa wananchi kufata maji umbali mrefu maji yasiyokuwa safi na salama.

Amesema mradi huo wa ujenzi wa kisima kirefu utawezesha kuzalisha maji lita 3,800 kwa saa hivyo wananchi watapa maji safi na salama ya kutosha katika eneo lao.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa nyumba ya mitambo, ufungaji wa pampu pamoja na mfumo wa umeme jua, uzio,ujenzi wa vituo 4 vya kuchotea maji pamoja na kuunganisha wateja majumbani.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe, Wilson Shimo wakati akizindua mradi huo ameipongeza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilaya ya Geita kwa kukamilisha ujenzi wa maradi huo.

Mhe, Shimo amesema kukamilika kwa mradi huo sasa wananchi wa kaseme wanakwenda kuondokana na kero ya ukosefu wa maji safi na salama katika eneo lao amewataka kuutunza mradi huo ili uweze kutumika kwa mda mrefu.

“Baada ya kuwa na huu mradi tuutunzeni tuuone kwamba ni mali yetu tukiutunza utadumu na tutapata maji miaka na miaka lakini niwambieni tukianza kuuchezea chezea mradi huu baada ya miaka michache huko mbeleni tutapata maji kidogo au kuisha kabisa” alisema Mhe, Wilson Shimo Mkuu wa wilaya ya Geita.

Previous articleHABARI PICHA: MATUKIO KUTOKA UWANJA WA MICHEZO WA NKURUNZIZA BURUNDI
Next articleBIBI ADAI KUTISHIWA MAISHA DODOMA, KUPOKWA SHAMBA LA HEKARI 14
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here