Home LOCAL SHAKA ATAKA MAJIBU MRADI WA MAJI ULIOKWAMA NANYUMBU.

SHAKA ATAKA MAJIBU MRADI WA MAJI ULIOKWAMA NANYUMBU.

NA: MWANDISHI WETU.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha mradi wa maji wa Nandete uliopo wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara unakamilika na kutoa huduma kwa wananchi.

Shaka ameeleza hayo baada ya kupata taarifa kuwa mradi huo hautoi huduma tangu Februari mwaka huu, baada ya pampu na jenereta kuungua.

Akitoa maelekezo kwa viongozi wa serikali na mamlaka husika za Mkoa wa Mtwara, Shaka amesema sababu zilizotolewa kuhusu kutofanya kazi kwa mradi huo haziingii akilini, hivyo alimuagiza mkuu wa Mkoa huo, Marko Gaguti kutumia vyombo mbalimbali ikiwemo TAKUKURU, kutafuta ukweli wa jambo hilo.

“Huu mradi nitabanana mimi na Serikali kuchukua hatua kwa yeyote aliyehusika kukwamisha kwa sababu sijaridhika na majibu ya mradi huu na CCM hatuwezi kukaa na watu wababaishaji.” Amesema Shaka alkizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mnanje B.

“Tumekagua mradi wa maji na Ilani ya uchaguzi ya CCM ibara ya 100 inasema tutasimamia usambazaji wa maji mijini na vijiji, ili uchumi ukue lazima tuboreshe huduma za kijamii na miongoni mwao ni huduma ya maji, maji ndio kila kitu.

“Serikali inachukua hatua kadhaa kuondoa changamoto ya maji na katika Mkoa wa Mtwara imeleta Sh. Bilioni 13.9 kwa lengo la kuimarisha upatikanaji maji. Tunataka ikifika mwaka 2025 utekelezaji wa Ilani iwe imefikia asilimia 95 na moja ya eneo ambalo tunataka kuona linafanikiwa ni maji,” alisema Shaka

Akizungumza na wananchi katika Kijiji Cha Mnanje, wilayani Nanyumbu, Shaka alisema anazo taarifa za kutosha za mradi wa maji Nandete, hivyo ametaka kupata majibu kabla ya kuondoka Mkoa wa Mtwara. 

“Nimepokea malalamiko mengi sana kuhusu huu mradi wa maji Nandete. Serikali ya Rais Samia na CCM itasimama na wananchi.

“Hatuwezi kuona watu wachache ambao wanaangalia maslahi yao binafsi wanakwamisha miradi ya maji. Huu mradi wa maji Natende nataka majibu yake na Mkuu wa Mkoa tumia vyombo vyako kupata taarifa na bahati nzuri taarifa zote ninazo. Kuna mambo mengi yamefanyika na hawasemi, kuna mambo mengi yamejificha,” amesema Shaka akitoa maelekezo baada ya kutembelea mradi wa maji wa Maratani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Gaguti, alisema amepokea maelekezo hayo na atakwenda kuyafanyia kazi huku akiahidi kutoa majibu kuhusu mradi wa maji Nandete.

Gaguti alisema haiingii akilini kusikia mashine ya kusukuma maji katika mradi huo wa Nandete iliyoharibika Februari mwaka na kuagizwa kutoka Dar es Salaam iwe haijafika kwa muda wote huo.

Awali akitoa maelezo kuhusu mradi wa maji Nandete, Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Simon Mchucha alisema umesimama kutoa huduma Februari mwaka huu baa ya pampu ya kuvuta maji pamoja na jenereta kuungua.

Aidha, alisema walichukua hatua ya kumtaka mkandarasi kununua pampu nyingine ambapo aliagiza kutoka Dar es Salaam lakini hadi sasa haijafika na wanendelea kuisubiri.

Previous articleSOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 3-2022
Next articlePOLISI GEITA YAWANASA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA UTAPELI WAKIJIFANYA MAAFISA WA SERIKALI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here