Home LOCAL RAIS DKT. MWINYI AONGOZA MJADALA KUKUZA UWEKEZAJI WA MAKAMPUNI YA ULAYA NCHINI

RAIS DKT. MWINYI AONGOZA MJADALA KUKUZA UWEKEZAJI WA MAKAMPUNI YA ULAYA NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti (kushoto) wakati alipowasili katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiteta na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti kabla ya mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti (wa pili kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Mustafa Kitwana (kushoto) kabla ya kuingia katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na wadau mbali mbali na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ( kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga (wa tatu kulia) wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika hafla ya mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali, Balozi wa Netherland Nchini Mhe.Wiebe de Boer (kushoto) Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti (wa pili kushoto) Balozi wa Netherland Nchini Tanzania Mhe.Wiebe de Boer na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga (wa tatu kulia) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Wadau na waalikwa mbali mbali wakiwa katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na Balozi wa Netherland Nchini Tanzania Mhe.Wiebe de Boer wakishuhudia Utiaji saini wa Ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi na Jumuiya ya Ulaya katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya Nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega Uchumi ZIPA Nd,Sharif Ali Sharif na (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji anaeiwakilisha Jumuiya hiyo Cikay Richards.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar ambapo wadau mbali mbali wamehudhuria katika mjadala huo.
Previous articleUJENZI WA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA DODOMA KUKAMILIKA 2023
Next articleVIJANA NCHINI KUWEZESHWA UFUGAJI KIBIASHARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here