Home LOCAL POLISI GEITA YAWANASA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA UTAPELI WAKIJIFANYA MAAFISA...

POLISI GEITA YAWANASA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA UTAPELI WAKIJIFANYA MAAFISA WA SERIKALI.

Na.Costantine James, Geita.

Jeshi la Polisi Mkoani   Geita linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutapeli wakijifanya maafisa kutoka serikalini.

Watu hao waliotambulika kwa majina ya Emmanuel John(38), Stanley George (34), na Musa Nasoro (35) wakazi wa Dar es salaam kwa tuhuma za kuwatapeli viongozi mbalimbali wa serikali wakijifanya ni maafisa kutoka ikulu.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amesema watu hao wamekamatwa kwa kujifanya maafisa wa serikali na kuwapigia viongozi mbalimbali wa serikali kwa lengo la kutaka kuwatapeli.

 Mwaibambe amesema Watuhumiwa hao walikuwa wanawapigia viongozi mbalimbali wa Serikali na kujitambulisha kuwa  ni wasaidizi kutoka ofisi ya Rais na kuwaeleza kuwa Rais anafurahishwa  na jinsi wanavyotenda kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here