Home LOCAL MWALIMU TUNDURU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE

MWALIMU TUNDURU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro wa pili kulia akiwa amemshika mototo mmoja kati ya watoto mapacha wanne wa Mwalimu  wa shule ya msingi Wenje kata ya Nalasi wilayani humo Judith Chawe,wa kwanza kulia Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Ombeni Hingi.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Julius Mtatiro wa tatu kushoto na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wakiwa wameshika watoto mapacha wa Mwalimu wa shule  ya msingi Wenye wilayani humo Judith Chawe wa kwanza kulia na mumewe Hamis Hamza Shaibu.

Na: Muhidin Amri, Tunduru

MWALIMU wa shule ya msingi Wenje kata ya Nalasi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Judith Chawe(29), amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya Misheni Mbesa wilayani humo.

Mwalimu Judith alisema kuwa,watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni wawili na wa kike wawili na alifungua kwa njia ya kawaida na wanaendele vizuri na kuongeza kuwa huo ni uzazi wake wa pili.

“Kwanza namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama,lakini kutokana na mahitaji makubwa ya watoto wangu nawaomba wasamaria wema na Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema wanisaidie mahitaji mbalimbali kama fedha na maziwa ili niweze kuwalea hawa watoto”alisema Mwalimu Chawe.

Alisema,wakati anahudhuria kliniki Madaktari walimweleza kuwa ana watoto watatu tumboni,lakini kumbe walikuwa wanne na kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto hao na ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Baba mzazi wa watoto hao Hamis Shaibu amemshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto wanne kwa mkupuo,hata hivyo ameiomba jamii iweze kuwasaidia kwa hali na mali mahitaji ya watoto hao.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amefika nyumbani kwa Mwalimu huyo ili kumjulia hali na kuwaona watoto hao ambapo amewaomba Watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia Mwalimu Judith ili aweze kuhudumia watoto hao wanaohitaji gharama kubwa.

Mtatiro alisema,watoto hao wanahitaji msaada na huduma ya karibu kwa sababu maziwa ya mama peke yake hayatoshelezi kuwahudumia watoto hao wote wanne.

Alisema,serikali itakuwa bega kwa bega na Mwalimu huyo ili uona maendeleo ya afya yake na watoto hao na amemwagiza Kai u Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru Ombeni Hingi, kuhakikisha Halmashauri inampatia gari Mwalimu huyo kila atakapohitaji kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya Mwalimu huyo na watoto wake.

Alisema,kazi ya malezi ya watoto wanne ni kubwa kwa hiyo lazima Serikali na jamii kums idia Mwalimu Judith katika malezi ya watoto hao waendele kukua vizuri na kuwa na afya njema.

Awali Afisa Tarafa wa Nalasi Salum Kijumu alisema, baada ya kupata taarifa ya Mwalimu Ju ith kujifungua watoto wanne wameanza utaratibu wa kumchan ia fedha kutoka kwa watumishi wanaofanya kazi katika Tarafa hiyo ili ziweze kusaidia mahitaji ya watoto hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here