Home SPORTS NAMUNGO YAICHAPA MTIBWA 4-2

NAMUNGO YAICHAPA MTIBWA 4-2

Mwandishi wetu

TIMU ya Mtibwa Sugar leo imejikuta wakati mgumu baada ya wapinzani wake Namungo  kutokea nyuma na kuichapa mabao 4-2.

Hata hivyo kiungo  mshambuliaji, Shiza Ramadhani Kichuya leo ameifungia mabao matatu  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Kichuya amefunga mabao hayo dakika za 24, 51 na 66 huku bao lingine la Namungo likifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 73, wakati ya Mtibwa yamefungwa na Nzigamasabo Steve kwa penalti dakika ya sita na George Makang’a dakika ya 10.

Namungo FC inafikisha pointi 40 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 31 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 29.

Previous articleMWALIMU TUNDURU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE
Next articleSAINI YA MAKUBALIANO UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here