MRATIBU wa Utalii Daniel Maragashimba ameongoza vijana 800 wa Umoja wa Vijana wa CCM safari ya KUTALII NGORONGORO pamoja na Katibu wa UVCCM Taifa .
MARAGASHIMBA mdau wa Utalii Tanzania Mshauri wa uendeshaji wa Biashara ya Utalii Hotel Peacock alisema dhumuni la safari hiyo kutangaza mbuga zetu Tanzania katika Utalii wa ndani pamoja na kukitangaza chama Cha Mapinduzi CCM.
“Tumeanza safari ya kwenda Mbuga ya NGORONGORO pamoja na Vijana 800 wa UVCCM na kiongozi wao wa UVCCM Taifa lengo la ziara hii kuunga mkono juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutangaza vivutio vyetu vya Utalii vya ndani kupitia kampeni ya Royal Tour “alisema Maragashimba.
Alisema katika safari hiyo Mkuu wa msafara Kiongozi wa umoja wa vijana wa UVCCM Taifa Kihogosi anapeperusha bendera ya chama kutangaza utalii katika mbuga ya Ngorongoro.
MARAGASHIMBA alisema nchi yetu ya Tanzania kuna mbuga nyingi za wanyama mbalimbali hivyo kila mtanzania anatakiwa kutenga siku Maalum kwa ajili ya kutembelea mbuga hizo kwa ajili ya Utalii wa ndani kuongeza pato la Taifa.
Alitaja baadhi ya mbuga za Tanzania zenye vivutio vya wanyama mbalimbali ambazo ni mbuga za Manyara,Tarangire,Mikumi, Serengeti,Udizungwa , NGORONGORO.
Mwisho.