Home BUSINESS MARAGASHIMBA AONGOZA VIJANA 800 WA UVCCM KUTALII NGORONGORO

MARAGASHIMBA AONGOZA VIJANA 800 WA UVCCM KUTALII NGORONGORO


NA: HERI SHAABAN, Herishaban@gmail.com

MRATIBU wa Utalii  Daniel Maragashimba ameongoza vijana 800 wa Umoja wa Vijana wa CCM   safari ya KUTALII NGORONGORO pamoja na Katibu wa UVCCM Taifa .

MARAGASHIMBA mdau wa Utalii Tanzania Mshauri wa uendeshaji  wa Biashara ya Utalii Hotel Peacock  alisema dhumuni la safari hiyo kutangaza mbuga zetu Tanzania katika Utalii wa ndani pamoja na kukitangaza chama Cha Mapinduzi CCM.

“Tumeanza safari ya kwenda Mbuga ya NGORONGORO pamoja na Vijana 800 wa UVCCM na kiongozi wao wa UVCCM Taifa lengo la ziara hii kuunga mkono juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutangaza vivutio vyetu vya Utalii vya ndani kupitia kampeni ya Royal Tour “alisema Maragashimba.

Alisema katika safari hiyo Mkuu wa msafara Kiongozi wa umoja wa vijana wa UVCCM Taifa Kihogosi anapeperusha bendera ya chama kutangaza utalii katika mbuga ya Ngorongoro.

MARAGASHIMBA alisema nchi yetu ya Tanzania kuna mbuga nyingi za wanyama mbalimbali hivyo kila mtanzania anatakiwa kutenga siku Maalum kwa ajili ya kutembelea mbuga hizo kwa ajili ya Utalii wa ndani kuongeza pato la Taifa.

Alitaja baadhi ya mbuga za Tanzania zenye vivutio vya wanyama mbalimbali ambazo ni mbuga za Manyara,Tarangire,Mikumi, Serengeti,Udizungwa , NGORONGORO.

Mwisho.

Previous articlePATA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 6-2022
Next articlePROF. MAKUBI AKUTANA NA NA KUZUNGUMZA NA MADAKTARI BINGWA MISRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here