Home LOCAL BODI YA WANAHABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI – AG FELESHI

BODI YA WANAHABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI – AG FELESHI

 PICHA ZOTE NA YUSUPH KATIMBA (TEF)

Na: YUSUPH KATIMBA (TEF), DODOMA.

Mwanasheria Mkuu wa Serilikali (AG) Jaji Mstaafu Dkt. Eliezer Fereshi, amependekeza kuwepo na bodi ya wanahabari itakayosimamiwa na wanahabari wenyewe ili kuratibu na kusimamamia masuala mbalimbali katika Tasnia hiyo.

Amesema, chombo hicho ndio kitachokuwa na wajibu wa kusimamia wanahabari na hata kuwashughulikia endapo watakwenda kinyume na maadili ya habari.

Jaja Fereshi ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Juni 2022, OIfisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma alipokutana na wadau wa habari.

“Sina tatizo, naona muwe na ‘regulator’, bodi yenu moja, ili mmoja wenu akienda kinyume na maadili (ya uandishi wa habari), mnamshughulikia nyinyi wenyewe,” amesema Jaji Eliezer Fereshi.

Aidha Jaji Fereshi ametoa kauli hiyo baada ya kupokea maelezo kutoak kwa  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alipomweleza kuwa, wanahabari  wanapendekeza kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia wanahabari badala ya vyombo vinne kama inavyoelekezwa na Sheria ya sasa.

Pia Balile amemweleza Jaji Fereshi kuwa, miongoni mwa mambo yanayowatisha wanahabari katika sheria iliyopo sasa ni uwepo wa kifungo bila hata ya muhusika kuitwa kusikiliza kesi yake.

Jaji Feleshi amesema, sheria yoyote lazima ipitiwe vizuri na iwe na uhalali lakini pia iwe ya wananchi.

Mwanasheria huyo amesema, Ofisi yake ipo pamoja na hatua zinazochukuliwa na wanahabari katika kuyaendea mabadiliko yanayotakiwa.

“Niko na nyinyi na Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) katika hatua kuelekea mabadiliko ya sheria za habari.

Previous articleKMC FC WAPO FITI KUIVAA PRISONS KESHO
Next articleBRELA YAZINDUA WIKI YA ‘SULUHISHA NA BRELA’ INAYOLENGA KUTATUA MIGOGORO YA KAMPUNI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here