Home BUSINESS BRELA YAZINDUA WIKI YA ‘SULUHISHA NA BRELA’ INAYOLENGA KUTATUA MIGOGORO YA KAMPUNI

BRELA YAZINDUA WIKI YA ‘SULUHISHA NA BRELA’ INAYOLENGA KUTATUA MIGOGORO YA KAMPUNI


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya Biashara (BRELA) Meinrad Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la kutatua na kusuluhisha migogoro ya Kampuni lililoanza leo Juni 13,2022 katika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Afisa sheria wa BRELA Vicensia Fuko (wa pili kulia) pamoja na Afisa Usajili wa Taasisi hiyo Angela Kimaro (kushoto) wakimsikiliza mteja aliyefika kwaajili ya kupata msaada wa Mgogoro wa Kampuni yake katika zoezi la siku tano la WIKI YA SULUHISHA NA BRELA linalofanyika kuanzia leo Juni 13,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Afisa Sheria wa BRELA Charles Kisanga (wa kwanza kushoto) na Afisa Usajili Angela Kimaro (wa pili kushoto) wakifuatilia maelezo ya mteja aliyefika kwaajili ya kupatiwa huduma katika zoezi hilo.
 
Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa BRELA Bi. Rhoida Andusamile akifuatilia kwa umakini moja ya suluhishi katika zoezi hilo.
Afisa Tehama wa BRELA Joram Manyika akitimiza majukumu yake alipokuwa akitoa huduma kwa mteja aliyefika kwenye Dawati lake katika zoezi hilo la siku tano Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.
 
Na: HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM.

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imezindua rasmi zoezi la kusuluhisha na kutatua migogoro ya Makampuni itakayohusisha kusikiliza kero na changamoto zao ili kuzipatia ufumbuzi ambapo zoezi hilo limepewa jina la WIKI YA SULUHISHA NA BRELA.
 
Zoezi hilo limeanza leo Juni 13,2022 katika ukumbi wa mikutano wa makumbusho ya Taifa uliopo katikati ya Jiji la Dar es  Salaam ambapo wananchi watapata fursa ya kukutana na maafisa wa BRELA kwaajili ya kueleza kero na migogoro iliyopo kwenye kampuni zao na kupatiwa ufumbuzi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungua rasmi zoezi hilo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Makampuni na majina ya Biashara (BRELA), Bw. Meinrad Rweyemamu amesema kuwepo kwa zoezi hilo kunawapa fursa wamiliki wa Makampuni yenye Migogoro mbalimbali kupata msaada wa utatuzi wa changamoto zinazowakabili.
 
“Zipo changamoto nyingi ndani ya Makampuni kuna wakati mwenye hisa hutokea amefariki huku ndugu hawafahamu kinachoendelea kwenye kampuni, hawafahamu hata kama zile hisa za marehemu ni mali kama mali nyingine zinapogaiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Njoo katika wiki hii tutakuwa pamoja, tutaangalia haki yako ni ipi”. Amesema Rweyemamu.
 
Na kukusisiza kuwa “Sisi kama BRELA ni lango la Biashara kwa hiyo kampuni inayozalishwa BRELA isipofanya vizuri inaamana lengo letu tunakuwa hatujalifikia hivyo katika hii wiki tunawakaribisha wamiliki wote wa makampuni kwaajili ya kuja kutatua changamoto zao” amesisiza.
 
Na kuongeza kuwa “Pia Kampuni inamilikiwa na watu hivyo unaweza kukuta ndugu yako au mzazi wako alikuwa na hisa, hizi ni mali kama mali nyingine na hisa zinahamishika hivyo wale wenye changamoto za namna hii njooni tutaangalia, tutakuelekeza na kukushauri hatua zipi za kufuata. ameongeza.
 
WIKI YA SULUHISHA NA BRELA iliyoanza leo Juni 13, 2022 inatarajiwa kuhitimishwa siku ya jumapili Juni 19,2022 ambapo migogoro mbalimbali ya Makampuni itapatiwa ufumbuzi.

Previous articleBODI YA WANAHABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI – AG FELESHI
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI (DIASPORA) WANAOISHI NCHINI OMAN
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here