Kaimu Meneja wa Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kupokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema, (katikati) kutokana na kampuni hiyo kuunga mkono Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katika jitihada zake za kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza sekta ya utalii nchini, kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa Bulyanhulu, imekuwa moja ya wadhamini wakuu wa Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililofanyika katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mbali na ufadhili kampuni iliwezesha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa kuweza kuona filamu maarufu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 6,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 7,2022.
Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo, Mhe. Mjema amewapongeza na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la utamaduni ili kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni zao kama Rais Samia anavyosisitiza mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuenzi utamaduni zikiwemo mila na desturi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja wa Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) akizindua Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa Old Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga. Kushoto aliyevaa tisheti nyeupe ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.
Wananchi wakiwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Skrini kubwa iliyoletwa na Kampuni ya Barrick katika kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa Old Shinyanga kwa ajili ya kuonesha Filamu ya The Royal Tour. Wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa walipata fursa ya kuona filamu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wakiwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ya Ngoma ya Wagoyangi wanaocheza na nyoka ikiendelea kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Akina mama kutoka Kishapu wakitwanga nafaka kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.