Kamishina wa Chama cha Skauti Wilaya ya Singida na Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akiwa kwenye sherehe ya Wazazi na Walezi wenye watoto wao ambao ni Skauti wilayani humo iliyofanyika jana
Mkuu wa Chuo cha VETA Mkoa wa Singida, Paul Batoleki ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Wazazi Wenye Watoto Skauti Manispaa ya Singida akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Judith Kweka akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mafunzo ya uzimaji moto yakifanyika katika hafla hiyo.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja meza kuu.
Na: Dotto Mwaibale, Singida.
MKUU wa Chuo cha VETA Mkoa wa Singida, Paul Batoleki ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Wazazi Wenye Watoto wa Skauti Manispaa ya Singida ,amewataka wazazi kuwalea watoto katika misingi ya uadilifu na uzalendo.
Batoleki amesema jamii ya sasa imesahau wajibu wao katika malezi ya vijana kama ilivyokuwa zamani, wazazi wamekuwa wakiangaika na majukumu mengine ya kiuchumi na kisiasa na kusahau jukumu muhimu la malezi ya watoto na vijana.
Batoleki alisema hayo katika Mkutano wa Siku ya Wazazi wenye Watoto wa Chama cha Skauti Manispaa ya Singida uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Chuo cha Ufundi VETA SIngida.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Kamishina wa Chama cha Skauti Wilaya ya Singida na Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani alisema Chama cha Skauti kimejikita kuwajenga vijana katika uzalendo na ukamamavu pamoja na mafunzo mbalimbali ya kujikinga na kujiokoa na majanga na Kupambana Kuzuia Rushwa
Ndahani alisema Skauti katika Wilaya ya Singida imeendelea kufundisha vijana juu ya elimu ya kujitegemea ikiwa ni pamoja na kujikita katika kilimo cha bustani na ufugaji wa Kuku,Bata,Njiwa na Sungura ili waweze kutumia mazingira vizuri na kujifunza namna ya kujitegemea.
kuzuia,Kuokoa na kupambana na majanga ya moto kutumia vifaa vya kisasa yaliyotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida.
Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi Judith Kweka alisema amekishukuru chama cha Skauti kwa ushirikiano mkubwa wanaopata katika kutoa elimu ya kujikinga na majanga ya mbalimbali ikiwemo moto, na ameshauri walimu kuwatumia vijana wa skauti kutoa elimu ya majanga ya moto kwa kuwa wanamafunzo ya kutosha ya kuzima moto .
Aidha amewaomba wananchi kununua vifaa vya kujikinga na kuzuia majanga ya moto kwani nyumba na mali zina thamani kubwa ukilinganisha na bei za vifaa hivyo.
Kwa niaba ya wazazi Mzee Juma Mohammed alisema amefurahi kujifunza namna ya kuzima moto ambapo toka azaliwe hajawahi pata nafasi ya kujifunza namna ya kuzima moto.
Siku ya Wazazi wenye Vijana wa Skauti hufanyika kila mwaka ikiwa na lengo la kuimalisha uhusiano kati ya Wazazi na Chama hicho pamoja na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vijana wa Skauti.