Home LOCAL DC IKUNGI AONGOZA MAZISHI YA MTOTO ALIYE UAWA NA TEMBO

DC IKUNGI AONGOZA MAZISHI YA MTOTO ALIYE UAWA NA TEMBO

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry. Muro jana Mei 27/2022 amewaongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Ntuntu kijiji cha Ntuntu Kitongoji cha Wangama katika mazishi ya mtoto Zaurati Japhari Shaban mwenye miaka miwili na miezi nane alieuwawa na Tembo majira ya asubuhi saa mbili walipokwenda kuteka maji na mama yake

 
MKUU  wa Wilaya ya Ikungi Jerry. Muro jana Mei 27/2022 amewaongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Ntuntu kijiji cha Ntuntu Kitongoji cha Wangama katika mazishi ya mtoto Zaurati Japhari Shaban mwenye miaka miwili na miezi nane alieuwawa na Tembo majira ya asubuhi saa mbili walipokwenda kuteka maji na mama yake.
 
DC Muro ambae amelazimika kusitisha shughuli zake na kuelekea eneo la tukio ametoa pole kwa wazazi wa marehemu na wananchi wa kata ya Ntuntu na kuwahakikishia wananchi kuwa wataalam wa idara ya wanyamapori wataweka kambi katika eneo hilo mpaka hapo hatima ya tembo huyo itakapojulikana  Mara baada ya mazishi DC Muro akiwa pamoja na wataalam wa wanyamapori kutoka kambi ya manyoni wameendelea na msako wa tembo huyo ili asilete madhara zaidi kwa wananchi.
 
Previous articleWAZAZI SINGIDA WAHIMIZWA KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA.
Next articleKONGAMANO LA AIESEC LAFANYIKA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here