Home BUSINESS TFS KANDA YA KUSINI YAWAKUTANISHA WATAALAM NA WADAU WA SEKTA YA MISITU...

TFS KANDA YA KUSINI YAWAKUTANISHA WATAALAM NA WADAU WA SEKTA YA MISITU KANDA YA KUSINI WAKUTANA KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA MISITU NA NYUKI

Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akifungua mkutano wa wataalam wa misitu kutoka mikoa ya kusini Lindi,Mtwara na Ruvuma uliofanyika mjini Lindi,katikati kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Lindi Dkt Dora Haule,

Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Lindi Dkt Dora Haule akizungumza na wataalam na wadau wa sekta ya misitu kutoka mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kwenye mkutano wa kutafuta na kuboresha sekta ya misitu na nyuki katika mikoa hiyo,

Kamanda wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)kanda ya kusini Kamishina msaidizi Manyise Mpokigwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa sekta ya misitu na nyuki kwa washiriki wa mkutano wa wataalam wa sekta ya misitu kanda ya kusini,

Afisa Misitu Daraja la 1 wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)Kanda ya kusini Rweyemamu Kamugisha akizungumza katika mkutano wa wataalam wa misitu uliofanyika mjini Lindi.

Afisa Misitu Mkuu kutoka wizara ya Maliasili na Utalii James Nshare akizungumza katika mkutano huo.

Afisa Maliasili wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Ombeni Hingi akizungumza wakati wa mkutano wa wataalam wa misitu wa mikoa ya Kusini.

Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)kanda ya kusini na wadau na wataalam wa sekta ya misitu kutoka mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma.

Na: Muhidin Amri, Lindi

MKUU wa mkoa wa Lindi Zainab Teleck,amewataka wadau wa misitu kanda ya kusini kuunganisha nguvu zao ili kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa misitu, kulinda uoto wa asili ili kuwa na misitu endelevu kwa ajili ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.


Teleck ametoa kauli hiyo jana,katika Hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wataalam wa misitu Kanda ya kusini uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Lindi.

Taleck alisema, uharibifu wa misitu usipodhibitiwa utasababisha gharama kubwa ya kurejesha uoto wa asili ulioanza kupotea na hata kusababisha kizazi kijacho kushindwa kupata matunda ya misitu iliyopo hapa nchini kutokana na tamaa ya baadhi ya watu wachache kutaka kujinufaisha wao binafsi.

Alisema,pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali  kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) kanda ya kusini na wadau mbalimbali katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira,lakini bado kuna kiwango kikubwa cha uhabifu wa mazingira ikiwamo tatizo la ukataji miti ovyo na uchomaji moto misitu hasa ya asili jambo linalotishia kwa kiwango kikubwa upotevu wa misitu.


Kwa mujibu wa Mkuu  wa Mkoa ni kwamba Mkoa wa Lindi na Mikoa mingine ya Kanda ya Kusini ina Utajiri Mkubwa wa Rasilimali Misitu, hata hivyo pamoja na Juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ili kuhifadhi rasilimali Misitu kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Halmashauri za Wilaya na wadau mbalimbali  na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  ikiwamo Shirika la Mpingo (MCDI), FORVAC, WWF, TFCG na Mjumita  bado tunakabiliwa na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Misitu kutokana na matumizi yasiyo endelevu.

Aidha, amewapongeza waandaaji wa Mkutano huo (Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya kusini na Shirika la Mpingo (MCDI) kwa adhma ya kuwakutanisha Watalaam ili
kujadiliana juu ya namna bora ya kuimarisha Usimamizi wa Misitu katika Kanda ya Kusini.

Alisema, kuna tabia mbaya inayofanywa na Wananchi wanaofyeka Misitu kwa ajili ya kilimo cha kuhamahama, uchomaji moto hovyo, ufugaji ndani ya Misitu ya Hifadhi na uvunaji usiofuata Mpango wa Uvunaji.


Telack amewataka wadau na wataalam  kutafuta namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo ili kunusuru rasilimali  za Misitu ambayo ni muhimu  katika kuchangia pato la Taifa, vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za matumizi yasiyo endelevu ya misitu ikiwamo uchomaji moto ovyo, kilimo cha kuhamahama na kuchunga mifugo ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Alisema,kwa sasa sekta ya Misitu inachangia asilimia 3.5% ya pato la Taifa ni dhahiri kuwa sekta ya Misitu ni fursa mojawapo ambayo ikitumika kikamilifu itachangia zaidi katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Lindi, Mikoa yote ya Kanda ya kusini na Taifa kwa ujumla.


Alieleza kuwa,Misitu ina fursa nyingi za Utalii, hivyo  ni muhimu kwa wataalam na wadau wa misitu  kupanga namna nzuri zaidi ya kuboresha na kuvitangaza vivutio vya Utalii na fursa zingine katika rasilimali Misitu ili kuchangia na kuunga mkono juhudi  za Mh. Rais  Samia Suluhu Hassan za Kutangaza Utalii kupitia  Filamu ya Royal Tour.

“Naomba sana waandaaji, mjiwekee utaratibu wa kufanya vikao hivi mara kwa mara ili kuwa kuwakutanisha Watalaam kutathimini utekelezaji wa yale mliyokubaliana, kupanga nini kifanyike na kukabiliana na mambo yanayojitokeza”alisema Mkuu wa mkoa”

Naye Afisa Uhifadhi Mkuu wa wakala wa huduma za misituTanzania  anayeshughulikia masoko na usimamizi wa rasilimali za misitu Salehe Beleko alisema,lengo la mkutano huo kukutanisha wadau wote wa misitu kwa ajili ya kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya misitu kwa kuamini kwamba hakuna sekta inayoweza kusimama pekee yake bila kushirikiana na wadau wengine.

Alisema,TFS ina majukumu mbalimbali ikiwamo kuanzisha na kusimamia misitu ya hifadhi na hifadhi za nyuki za Serikali kuu,kuanzisha na kusimamia mashmba ya miti,kusimamia rasilimali za misitu na nyuki katika  ardhi,kusimamia utekelezaji wa sheria,seraza misitu na ufugaji nyuki,kukusanya maduhuli ya serikali,kutoa huduma za ugani(elimu y usimamizi wa misitu) na kufanya biashara ya mazao ya na huduma za misitu na ufugaji.

Alisema, changamoto kubwa katika usimamizi na utekelezaji wa sera na sheria za misitu changamoto kubwa ni uchomaji misitu ovyo wakati wa kiangazi unaosababisha kuungua kwa miti midogo ambayo ni muhimu kwa bioanuai,mahitaji makubwa ya mkaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na migogoro ya mipaka kati ya vijiji na misitu ya serikali kuu au kati ya misitu  ya vijiji na misitu ya Serikali .

Hata hivyo alieleza kuwa,TFS imejipanga kumaliza migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na vijiji kwa njia ya mazungumzo  na kutengeneza mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji,kutoa elimu  ya usimamizi wa misitu na madhara ya moto kwa jamii na kuhamasisha upandaji wa miti inayokuwa haraka kwenye mashamba yao itakayotumika kuvuna kwa ajili ya kutengeneza mkaa na matumizi mengine ya kawaida.

Kwa upande wake Kamanda wa wakala wa huduma za misitu  Tanzania kanda ya kusini Kamishina msaidizi Manyise Mpokigwa amewaomba wadau wa  misitu kushirikiana na TFS katika kutekeleza na kusimamia rasilimali za misiti na nyuki ili ziwe endelevu na kuchangia uchumi wa nchi yetu.
MWISHO.

Previous articleWANANCHI WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA
Next articleWAZAZI SINGIDA WAHIMIZWA KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here