Home ENTERTAINMENTS TANZANIA YAJIWEKA MGUU SAWA KUANDAA TUZO ZA MTV AFRIKA MWAKA 2023

TANZANIA YAJIWEKA MGUU SAWA KUANDAA TUZO ZA MTV AFRIKA MWAKA 2023

 

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo  Bw. Saidi Yakubu leo Mei 09, 2022 jijini Dodoma  ameongoza kikao cha awali  kati ya Wizara na Wawakilishi wa  Waandaaji wa Tuzo za MTV Afrika kutoka nchini Afrika Kusini kujadili kuhusu  Tanzania kuandaa Tuzo za Muziki za MTV (The MTV Africa Music Awards ) Kwa mwaka 2022/23.

 Katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Yakubu  ameeleza utayari wa wizara kushirikiana na Kampuni hiyo kwakua ni fursa kubwa ya kuitangaza  Tanzania  hasa katika kipindi hichi ambacho Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  imeweka juhudi katika kuitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na watalii wengi duniani kuja nchini.

“Kikao cha leo kimetupa fursa ya kuona namna gani Nchi yetu itafaidika na ujio wa Tuzo hizo, tumeona  wasanii wetu watapata nafasi  ya kujitangaza na kutangaza Sanaa ya Tanzania  Duniani, Kuna fursa pia ya kutangaza Nchi yetu katika Utalii hivyo tumepokea wazo na tutalijadili na kutoa  mrejesho wenye tija” Amesema Naibu Katibu Mkuu Yakubu.

Ameongeza kuwa wizara yake itafanya Mawasiliano na Wizara nyingine ikiwemo Maliasili na Utalii pamoja na wadau wengine ili kuona namna ya kufanikisha tukio hilo kubwa la Muziki Barani Afrika ambalo likifanyika litakaribisha takriban wageni  elfu 10 nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka MTV, Ndugu Kabelo Ngakane alisema kuwa wanavutiwa na Tanzania kwakua imefunguka katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara ya Muziki na Utalii, hivyo ni fursa ambayo MTV itaitumia kuitangaza zaidi ulimwenguni.

Ameongeza kuwa, kufanyika kwa Tuzo hizo kutatoa nafasi kwa Wasanii mbalimbali ikiwemo wanamuziki, wachezaji (Dancers) waandaaji wa Muziki, watangazaji kupata elimu  pamoja na ujuzi mbalimbali katika kukuza Sanaa zao.

Tuzo za  Muziki za MTV Africa zilianza tangu Mwaka 2008  ambapo Nchi kama South Afrika Nigeria, Ghana  Uganda na Nyingine zimeshaandaa Tuzo hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here