Home LOCAL SERIKALI KUWAPATIA ELIMU YA CHANJO YA UVIKO 19 VIONGOZI WA NACOPHA

SERIKALI KUWAPATIA ELIMU YA CHANJO YA UVIKO 19 VIONGOZI WA NACOPHA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter (katikati) aakiwa na wajumbe kutoka NACOPHA katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) na serikali kilichofanyika leo Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza jambo na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Alex Sanga katika kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akiongoza kikao kazi na Viongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kilichofanyika leo Jijini Dodoma

Na. WAF– DODOMA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe ametoa wito kwa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kutoa elimu katika konga za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ili kuongeza hamasa ya watu hao kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO-19

Dkt. Shekalaghe ametoa rai hiyo leo Jijini Dodoma alipofanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter aliyeambapatana na wajumbe wake ambapo amesema kuwa elimu sahihi ikiwafikia walengwa katika konga zao itasadia kuongeza idadi ya uelewa katika jamii na kuhamasisha watu kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa hiari kwa wingi.

Akizungumza Dkt. Shekalaghe amesema kuwa elimu sahihi ikitolewa wakapata asilimia 90 ya watu 7,000 waliochanja na ikatolewa taarfa sahihi kwa jamii itasaidia kuhamasisha watu wengine ambao awaishi na virusi vya ukimwi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko 19

“Hivyo sisi kama Serikali tutajipanga na kuhakikisha viongozi wa Baraza la NACOPHA tunawapatia elimu sahihi juu ya watu kupata chanjo ili waweze kwenda kuelimisha katika konga zilizopo katika jamii na uelewa juu ya watu kuhiari na kupata chanjo ya UVIKO-19”, Dkt. Shekalaghe.

Hata hivyo Dkt. Shekalaghe amesema kuwa wao kama Serikali watahakikisha wanapokea mawazo, ushauri na wapo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na Baraza la NACOPHA ili kulinda afya za watanzania.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la NACOPHA, Deogratius Peter amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa huduma ambazo wamekuwa wakizitoa katika baraza hilo hususani matibabu wanayopatiwa pamoja na huduma nyingine zinazolenga mtu anayeiahi na Virusi vya UKIMWI hapa nchini.

“Kumekua na muamko wa watu waishio na kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO-19 hivyo tunaomba serikali kuongeza nguvu kwenye utoaji wa elimu juu ya watu kupata chanjo ya Uviko 19”, ameeleza Peter

Peter ameongeza kuwa wako tayari kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika barala hilo ili kuweza kufikia malengo tarajiwa.

Previous articleWAZIRI MKUU AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)
Next articleTANZANIA YAJIWEKA MGUU SAWA KUANDAA TUZO ZA MTV AFRIKA MWAKA 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here