Home BUSINESS SERIKALI YAAHIDI KUKAMILISHA MAJADILIANO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAAHIDI KUKAMILISHA MAJADILIANO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

 

DODOMA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema wizara inafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuona hakuna mgongano wa kisheria kwenye Mradi wa Liganga na Mchuchuma. 

Pia amesema ndani ya muda mfupi ujao mradi huo utaanza utekelezaji wake.

Dk Kijaji ameyasema hayo bungeni wakati wa kujibu hoja zilizoibuliwa na wabunge wakati wa kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2022/23  ya Wizara ambayo yameidhinishwa na Bunge Mei 9, 2022

“Nipongeze timu yetu ya kitaifa ya majadiliano imefanya kazi yake nzuri na sasa jambo hili lipo mikononi mwa Waziri wa Uwekezaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunaliahidi Bunge lako tukufu tunakwenda kuhitimisha  na Mwekezaji na taifa litaendelea kuwa salama” Amesema Dkt. Kijaji.

Na nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge wa Ludewa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inafanya kazi kuona hakuna mgongano wa sheria hizi mbili, sheria ya ardhi na ya uthamini ili tufike hatua njema kwa ajili ya wananchi wetu,” 

“Jambo ambalo naweza kukuahidi ni kwamba Wizara na Mthamini Mkuu wa Serikali tutafanya ziara na kuzungumza na wananchi wa vijiji hivyo viwili ili tuhitimishe jambo hili kwa mafanikio kati serikali, wananchi wetu na Mwekezaji. Hivyo nikutoe shaka tupo tayari kwa muda mfupi mradi huu utaanza utekelezaji wake.” 

Mapema, Akichangia Mbunge wa Viti Maalum, Neema Mgaya(CCM), aliomba serikali kuzungumza na Mwekezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili ufanye kazi na kuwa na viwanda vingi vya kuzalisha chuma Ili kupata material mengi ya chuma kwa ajili ya kuzalisha nondo kutengeneza mabati, misumari ili tusiwe na uhaba wa malighafi hii ili watanzania tunufaike nayo.

Previous articleTANZANIA YAJIWEKA MGUU SAWA KUANDAA TUZO ZA MTV AFRIKA MWAKA 2023
Next articleWAZIRI BASHUNGWA AMALIZA MGOGORO WA ENEO ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA MOSHI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here