Home LOCAL MADIWANI MKALAMA WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO

MADIWANI MKALAMA WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, James Mkwega akiongoza kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo leo.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akizungumza kwenye kikao hicho.

Madiwani wa Viti Maalumu, Zainabu Kihara kutoka Kata ya Kinyangiri (kushoto) na Wankembeta Timotheo kutoka Kata ya Ibaga wakipitia taarifa katika kikao hicho.

Baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.

Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Oliva Mgeni akijibu maswali kwenye kikao hicho.

Diwani wa Kata ya Ibaga, Salum Abdallah akiuliza ukamilikaji wa ujenzi wa Zahanati kwenye kijiji hicho.

Wenyeviti wa kamati mbalimbali wakiaga rasmi baada ya muda wao wa kutumikia kamati hizo kumalizika.


Mratibu wa Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi wa wilaya hiyo, Daniel Tesha akichukua maelezo kutoka kwa madiwani baada ya kutoa taarifa ya zoezihilo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira akizungumza kwenye kikao hicho.

Na: Dotto Mwaibale, Singida

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida wametakiwa kutoridhika na Sh.Bilioni 1.5 zinazokusanywa kwa mwaka badala yake waongeze  jitihada za kusimamia ukusanyaji ili  kuongezeka mapato.  

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo James Mkwega katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo leo.

Mkwega alisema uhitaji wa bajeti yao ni mkubwa mno kuliko  makusanyo hayo hivyo wasibweteke wakidhani ni fedha nyingi kwani zipo halmashauri zingine wanakusanya mapato zaidi ya Sh. Bilioni 5 hadi 30 akitolea mfano Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kueleza kuwa hata atapokuwa kwenye vikao vya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania huwa anachagua wenzake wa kukaa nao wanaolingana katika ukusanyaji wa mapato.

“Ni lazima tukusanye mapato na vyanzo vyetu vipo kwenye maeneo yenu madiwani tusikubali yakatoroshwa na kila unapokubali yatoroshwe unajiibia maendeleo kwenye kata yako hivyo kila mmoja akijihakikishia kulisimamia jambo ili kwa kukaa kwenye mageti kujiridhidha kama mazao yanayosafirishwa kama yamekatiwa ushuru hasa ya vitunguu na mengine itasaidia kuiongezea mapato halmashauri yetu” alisema Mkwega. 

Alisema mapato hayo ndiyo yanayoisaidia halmashauri kujenga vituo vya Afya, Zahanati  na miradi mingine ya maendeleo. Mkwega aliwaomba madiwani waliopo kwenye mageti makubwa kusaidia kudhibiti upotefu wa mapato hayo hasa katika maeneo ya Iguguno, Ibaga, Singa, kidalafa na sehemu zingine. 

Aidha Mkwega aliwahimiza viongozi wa vijiji na vitongoji na kata kusimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini ya mchanga kwa kuwaomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana na vijiji husika unapochimbwa mchanga huo au vifusi kwa ajili ya kulipa ushuru ambao ni uti wa mapato katika halmashauri hiyo.

Akizungumzia kuhusu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mkwega aliwaomba waratibu wa zoezi hilo kuweka nguvu ya kutoa elimu kwa wananchi wa kabila la Waazabe ambao wapo katika wilaya hiyo ambapo iwapo hawatachukua hatua za makusudi kulingana na mazingira wanayoishi wanaweza wasipate takwimu halisi na kujikuta wakikwama.

Hata hivyo Mratibu wa zoezi hilo wilayani humo Daniel Tesha alimuondoa wasiwasi kwa kumueleza kuwa umewekwa utaratibu mzuri kwa wananchi hao kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Asia Messos aliwahimiza wasimamizi wa zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi kuhakikisha linakamilika kwa wakati ndani ya muda uliopangwa kwani linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Lameck Mtungi alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mpango wa kuutangaza utalii wanchi yetu kupitia Filamu ya Royal Tour Tanzania ambayo ilizinduliwa nchini Marekani huku akisisitiza kuwa huwezi kufanya biashara bila ya kujitangaza.

Mbunge wa Iramba Mashariki Francis Isack aliiomba halmashauri hiyo kuandika andiko la kuomba ujenzi wa soko la kawaida na la vitunguu litakaloisaidia kupata mapato ambapo pia aliwapongeza madiwani kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia miradi ya maendeleo.

“Katika baraza hilo madiwani walipata fursa ya kuuliza maswali ya papo kwa papo na kujibiwa ambapo pia wenyeviti wa kamati mbalimbali walitoa taarifa ya maeneo wanayoyasimamia na kuyajadili kwa pamoja.

Previous articleBASHUNGWA ATAKA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A NA B KUTOLEWA SEHEMU MOJA
Next articleKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU YAELEZA MAFANIKIO ZIARA YA RAIS MAREKANI, ROYAL TOUR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here