Home BUSINESS BASHUNGWA ATAKA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A NA B KUTOLEWA SEHEMU ...

BASHUNGWA ATAKA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A NA B KUTOLEWA SEHEMU MOJA

KIGOMA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent L. Bashungwa(Mb)  amesema kuna haja ya Wizara yake pamoja na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kuangalia jinsi ya kuunganisha  utoaji wa leseni Kundi A na B ili kuepuka kuwachanganya wafanyabiashara.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo alipotembelea banda la BRELA Mei 11, 2022, katika maonesho ya Biashara yanayoendelea mkoani Kigoma.

Mhe. Bashungwa amesema utoaji wa leseni  za biashara kundi A zinazotolewa na BRELA  na zile za kundi B zinazotolewa na halmashauri zinawachanganya wafanyabiashara.

“Kuna haja ya wizara hizi kukaa pamoja na kuangalia uwezekano utakaowezesha leseni hizi kutolewa sehemu moja tofauti na ilivyo sasa,” amefafanua Mhe. Bashungwa.

Mhe. Bashungwa ambaye amefunga kongamano la biashara na kutoa tamko la kuongeza siku mbili za  maonesho  yanayoshirikisha wafanyabiashara kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Zambia, Congo na Tanzania amesema atazungumza pia na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA  kuhusu jambo hilo.

Previous articleCELINA GOMBANILLAH, MFANYAKAZI BORA MGODI WA BULYANHULU ANAYEAMINI UUGUZI NI KAZI YA WITO
Next articleMADIWANI MKALAMA WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here