Home LOCAL WATU 7 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI MJI MDOGO WA KATORO GEITA.

WATU 7 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI MJI MDOGO WA KATORO GEITA.

 

Na: Costantine James, Geita.

Watu saba (7) wakazi wa mji mdogo wa karoto wilayani Geita mkoa wa Geita wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa vitu mbalimbali ikiwemo  Tv, Magodoro,vyombo vya ndani, simu, sofa, Sora na vitu vingine mbali mbali.

Watu hao wamekamatwa kufuatia oparasheni  inayofanyika katika mji mdogo wa katoro wilayani Geita na jeshi la polisi jamii baada ya wizi  wa vitu mbalimbali vya ndani  kukisili katika mji mdogo wa katoro.

Jonathan Kazungu mwenyekiti wa kitongoji  mtaa wa  afya amesema wameamua kufanya oparesheni ya kuwasaka wezi hao katika mji mdogo wa katoro kutokana na wakazi wengi wa mji huo  kuripoti kuibiwa vitu vyao mbali mbali kiwemo Tv, Magodoro,vyombo vya ndani, simu, sofa, Sora na vitu vingine mbali mbali.

Jonathan ameliomba jeshi la polisi mji mdogo wa katoro  kushirikiana na viongozi mbalimbali wa vitongoji katika mji mdogo wa katoro kwa lengo la kuwabaini wezi hao.

“Tunaliomba jeshi la polisi lizidi kutupa ushirikiano pale tunapokuwa tumewabaini watu hawa mahakama yenyewe ambayo ni mhimili wa sheria waweze kutiwa mbaroni  ili tuweze kuliondoa tatizo hili katika jamii yetu.” Amsema Jonathan Kazungu.

Kamanda Mkuu wa polisi jamii kata ya Ludete Zabron Peter amesema  wameamua kufanya zoezi hilo la kuwasaka wezi  katika mji mdogo wa katoro kutokana na wizi kuongezeka kila kukicha.

Amesema katika kufanya zoezi hilo wamekamata vitu mbalimbali vilivyoibiwa  ambavyo ni Pikipiki,Sabufa,Simu, Tv, Magodoro pamoja na vitu vingine mbali mbali.

Baadhi ya Wakazi wa Mji mdogo wa katoro wamekili kuibiwa vitu vyao mbali mbali huku wengine wakiona baadhi ya vitu vyao vilivyokamatwa katika oparesheni hiyo.

Mayala John mkazi wa Mtaa wa Afya ni miongoni mwa watu  saba(7) walio kamatwa kwa tuhuma za wizi amekili  kujihusisha na vitendo vya wizi huku akisema huwa wanfanya wizi usiku watu wakiwa wamelala. 

Amesema chanzo cha kufanya hivyo ni ugumu wa maisha hali iliyosababisha wao  kujihusisha na wizi wa vitu hivyo.

“Kazi hii mimi kwakweli sasa huvi ninamwaka mmoja nafanya hii kazi ni katika maisha, maisha yenyewe magumu zaidi” Amesema Mayala John Mkazi wa mji mdogo wa Katoro Geita.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe zinaendelea kudhibitisha kwa tukio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here