Home BUSINESS WAKULIMA WA ZAO LA ALIZETI WAMESHAURIWA KUHAKIKISHA WANAKAGUA MASHAMBA YAO MARA KWA...

WAKULIMA WA ZAO LA ALIZETI WAMESHAURIWA KUHAKIKISHA WANAKAGUA MASHAMBA YAO MARA KWA MARA

Mtendaji mkuu wa wakala wa mbegu za Kilimo nchini ASA Dkt.Sophia Kashenge akikagua zao la Alizeti katika Shamba la Kilimi wilayani Nzega Mkoani Tabora


Na: Lucas Raphael,Tabora

Wakulima wa zao la Alizeti wameshauriwa kuhakikisha wanakagua mashamba yao mara kwa mara ili kubaini wadudu waharibifu ambao wamekuwa wakishambulia mbegu za zao hilo ili waweze kuwadhibiti mapema kwa kunyunyizia dawa kwani wadudu hao wamekuwa wakiathiri uzalishaji wa zao hilo.

Hayo yalibainishwa na Mtendaji mkuu wa wakala wa mbegu za Kilimo nchini ASA Dkt.Sophia Kashenge mbele ya wajumbe wa bodi ya ASA walipotembelea shamba la mbegu Kilimi lililopo wilayani Nzega Mkoani Tabora jana.

Alisema kwamba wakulima wanatakiwa kuangalia mara kwa mara mazao yao ili kuweza kujiepusha na wadudu waharibifu ambao wamekuwa ndio chanzo cha kupunguza wingi mbegu za mafuta kwenye mashamba mengi ya wakulima .

Dkt Sophia Kashenge alisema kwamba mbegu za alizeti aina ya Record C1 ni mbegu bora inatoa mafuta mengi lakini inatakiwa ungalizi wa karibu ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa mazao ya mafuta .

“Hii mbegu ya Record C1 ni mbegu bora sana kwa wakulima na utoa mafuta mengi hivyo inapaswa kuangaliwa kwa ungalifu ili mkulima aweze kunufaika kwa kupata mafuta mengi ambayo yatainua kipato cha mwananchi na kukuza uchumi wa jamii”alisema Dkt Sophia

Mtendaji huyo wa ASA aliwaeleza wajumbe hao wa bodi kwamba zao la Alizeti kwenye shamba la kilimi walipanda ekari 200 ambapo wanatarajia kuvuna mbegu tani 60 .

Aidha wajumbe hao walishuhudia uzalishaji huo mkubwa wa mbegu za mahindi aina ya T 105 walipanda kwenye ekari 108, na matarajio ni kuvuna tani 150 hadi 200 ,Mtama aina ya Macia uliopandwa kwenye ekari 75 na matarajio ni kuvuna tani 45 .

Hata hivyo mwenyekiti wa bodi ya wakala wa mbegu za kilimo ASA, Dkt Ashura Kihupi aliwapongeza wakala wa mbegu za kilimo bora za Kilimo nchini kwa kuamua kuwekeza kwenye shamba hilo kitu ambacho kinatoa tija kwa wakulima wa ukanda wa ziwa na Magharibi ya Tanzania .

Aidha alitoa wito kwa wawekezaji wengine nchini kujitokeza kuzalisha mbegu katika shamba hilo ili kuongeza upatikanaji wa mbegu za bora za kilimo.

Awali meneja wa shamba la wakala wa Mbegu Kilimi Nzega mkoani Tabora, Jacob Chiwanga aliwaeleza wajumbe wa bodi hiyo kwamba tani 350 za mazao mbalimbali zilisambazwa nchini kupitia kituo hicho katika msimu wa kilimo wa 2021-2022 .

Alisema kwamba Mbegu za mazao yaliyosambazwa na kuuzwa ni pamoja na Mahindi,Mtama,Alizeti,Ufuta,Mpunga na mbegu za mazao ya Mbogamboga .

Alisema kwamba lengo lilikuwa ni kuuza na kusambaza Tani 500 lakini kutokana na uhaba wa mvua za masika mwaka huu lengo limeshindwa kufikiwa hivyo wanajipanga katika msimu ujao wa kilimo wanatarajia kufikia malengo ya wakala wa mbegu nnchini .

Mwisho

Previous articleWATU 7 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI MJI MDOGO WA KATORO GEITA.
Next articleTAASISI ZA KIFEDHA ZIBUNI HUDUMA NAFUU KWA WATANZANIA – MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here