Home LOCAL WARATIBU WA IDSR NCHINI WAMETAKIWA KUZINGATIA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA ...

WARATIBU WA IDSR NCHINI WAMETAKIWA KUZINGATIA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume akuzungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa IDSR Taifa wakati wa kuufunga, Jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume akibonyeza kitufe katika kuzindua mfumo mpya wa ulioboreshwa wa teknolojia ya Android
Mwakilishi wa Wizara ya TAMISEMI-Afya, Bw. Gerald Mannase akimkabidhi tuzo ya ushindi kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume kwa niaba ya Mraribu wa IDSR wa Mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume akimkabidhi tuzo ya ushindi kwa Mkoa wa Mwanza, ikipokelewa na Mratibu msaidizi wa mkoa huo, Bw. Novatus Kitowile.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume akimkabidhi tuzo ya ushindi kwa Mkoa wa Arusha, ikipokelewa na Mratibu msaidizi wa mkoa huo, Bi. Debora Masaka.

Baadhi ya Waratibu wa IDSR Taifa wakiwa kwenye mkutano huo.
Washiriki na picha ya pamoja na Mgeni rasmi.

Na WAF, Dar.

WARATIBU wa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa ya milipuko na yale yaliyopewa kipaumbele kama ilivyoainishwa katika IDSR (Integrated Diseases Surveillance Response), wametakiwa kuzingatia ukuaji wa Teknoloji ili kwenda na wakati katika uwasilishaji wa ripoti zao.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume, wakati alipokuwa Mgeni rasmi katika kufunga mkutano mkuu wa mwaka wa IDSR ulienda sambamba na kuzindua mfumo mpya ulioboreshwa kuendana na muongozo wa tatu wa IDSR ulio katika teknolojia ya USSD na ule wa teknolojia ya Android,kwa Waratibu hao kutoka Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara, Mkutano uliofanyika  kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.

Awali akitoa neno kwa washiriki hao, Dkt. Mfaume amebainisha kuwa, Nchi ina mfumo wa eIDSR ambao ndo mfumo wa utoaji wa taarifa za magojwa yaliyopewa kipaumbele na ya milipuko hivyo Waratibu hao wanatakiwa kufuata kanuni husika za miongozo wa utoaji wa taarifa za magojwa kwa wakati.

“Miongozo ipo mingi sana, lakini sio wote wanaosoma miongozo hivyo kwa uzinduzi huu mpya wa mfumo wa eIDSR ulioko katika Android na USSD iliyoboreshwa, utasaidia kuboresha taarifa zetu kwa usahihi wake na kwa wakati.

Hivyo hakutakuwa na haja ya kusukumana kwenye kutuma taarifa”. Alisema Dkt. Mfaume.

“Tunataka takwimu ambazo tunazikusanya na kuzitolea taarifa, sisi wenyewe ambao tunazikusanya ndio tuwe watumiaji wa kwanza wa hizo taarifa. Nyie kama Waratibu wa IDSR, sehemu  yenu fulani inatawaliwa na mitandao ya kijamii (Social media), kwa sasa tunakimbizana na teknolojia, lakini ukiichelewa tu, inakuacha hivyo usingojee jambo asukumiwe Waziri kutoka kwa Wananchi huko ndio tuchukue hatua tujiongeze kwenye teknolojia,” alisema Dkt. Mfaume.

Na kuongeza kuwa;

“Mimi naona mnafanya kazi nzuri, na mimi naomba niwapongeze sana kwa yale Majedwali mnavyoyajaza.

Magonjwa 34 ambayo yapo kwenye mfumo huo mpya, kuna maeneo mengine hayatokei kwenye mikoa yenu, ila kuna magonjwa mengine tunayakosa kwa sababu hatuyafuatilii, twendeni tukayafanyie kazi mafunzo tuliopatiwa hapa,

tusisubirie mitandao ya  kijamii ndo ifanye kazi zetu ikiwemo kuripoti  taarifa za magonjwa huko mitaani.” Alisema Dkt. Mfaume.

Kwa upande wake Mratibu wa IDSR kitaifa Dr. Frank Matullu alibainisha kuwa;

Taarifa hizo za IDSR ni muhumu sana kwa kuwa ndo mfumo pekee unaotoa hali ya magojwa ya milipuko na yale yaliyopewa kipaumbele kila siku, hivyo upatikanaji wa taarifa kupitia mfumo wa eIDSR itasaidia Wizara kuwa na taarifa sahihi za mwenendo wa magojwa nchni.

Dkt. Frank Matullu aliongeza kuwa:

“Awali tulifanya mafunzo kwa muongozo wa pili wa IDSR nchni nzima na sasa mafunzo ya muongozo wa tatu yamefanyika katika mikoa 18 na mafunzo yanaendelea, mafunzo hayo yanajumuisha waratibu wa Mikoa na Wilaya pamoja na watoa taarifa ngazi ya kituo yanasaidia kuwapa uelewa wa pamoja mambo yaliyomo katika muongozo huo.

Ambapo pia aliipongeza mikoa 5 kwa kufanya vizuri  katika IDSR na kutunukiwa tuzo.

“Mikoa mitano ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Njombe, Mwanza na Geita ambayo imefanya vizuri tunaipongeza kwa kuwazawadia Tuzo ambazo itakuwa ni ishara ya Wizara kuwatambua na kuwapa muamko mikoa isiyofanya vizuri ili nayo mwaka unaokuja nayo ifanye vizuri.” Alisema Dkt.Frank.

Kwa upande wake Mratibu wa mkutano huo, Fidelis Ronjino alieleza kuwa, Mkutano  huo wa mwaka ambao huwa unafanyika kila mwaka kwa kuwaita Waratibu wa IDSR nchi nzima, na kabla ya hapo ulifanya miaka ya nyuma.

“Kwa sasa ni kama tumeianza kuhakikisha tunafanya vikao hivi vya mwaka vya IDSR kwa ajili ya kupitia mwenendo wa magonjwa nchini.

Ikiwa hasa kuweka mikakati ambayo itasaidia upatikanaji wa taarifa za magonjwa nchi nzima, kwa kitaifa lakini pia mapema zaidi ili Wizara ichukue hatua za haraka.”  alisema Fidelis.

Ambapo aliongeza kuwa, Waratibu walizingatia wale ambao kiutoaji wa taarifa wamefanya vizuri, lakini pia wakachukua mikoa ambayo hawafanyi vizuri michache ili iwe chachu ya kujifunza kwa yale ambayo  wenzao wanaofanya vizuri.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki na washindi wa mikoa katika IDSR wakitoa maoni yao:

Kwa upande wake Bi.Debora Masaka ambaye amemwakilisha Mratibu wa IDSR mkoa wa Arusha, amewashukuru Wizara ya Afya kwa kuandaa mafunzo hayo,ikiwemo kuandaa tuzo kwa mikoa inayofanya vizuri na mikoa mingine ambayo haifanyi vizuri wameomba iendelee kuwezeshwa

Katika kubadirishana mawazo na uwelewa kwa washiriki, ambapo amesema itasaidia kwao kuimarika katika ufuatiliaji wa magonjwa kwa manufaa ya taifa.”  Alisema Bi Debora.

Nae mwakilishi wa IDSR Mkoa wa Mwanza,Mratibu msaidizi wa IDSR, Bw. Novatus Kitowile aliyemwakilisha  Mratibu wa IDSR wa Mkoa huo wa Mwanza,  alisema;

“Kwa uwasilishaji wa data kwa muda muafaka tumeweza kupata zawadi kama Mkoa.

Tunawashukuru uongozi wa Wizara, wadau wote ikiwemo wadau wa maendeleo CDC, tutaendelea kujitahidi na kuwa wa kwanza zaidi na zaidi kuweza kutoa taarifa za magonjwa ya IDSR.” Alisema.

Mfumo huo wa kisasa wa uwasilishaji wa ripoti nchini,umekuwa na manufaa makubwa ambapo Waratibu hao wa IDSR hutumia vifaa vya kisasa ikiwemo simu za mkononi (smartphone ) na Kishkwambi pamoja na  Computer.

Ambapo mkutano huo, umewezeshwa kwa pamoja na Wizara ya Afya, Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wadau wa Maendeleo CDC  na wengine.

Mwisho.

Previous articleSPIKA WA BUNGE DKT. TULIA ACKSON AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KWA KUJIBU MASWALI VIZURI BUNGENI
Next articleSERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAKAZI BORA KWA WAHUDUMU WA AFYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here