Home LOCAL SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAKAZI BORA KWA WAHUDUMU WA AFYA

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAKAZI BORA KWA WAHUDUMU WA AFYA

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha makazi ya wahudumu wa afya nchini ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 imejenga nyumba 176.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali la Mbunge Mhe. Nora Waziri Mzeru (Viti Maalum) aliyeuliza Mpango wa Serikali kuwajengea nyumba wahudumu wa kada mbalimbali za afya na kuboresha makazi.

Dkt. Mollel amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali itajenga nyumba 300 za kukaa familia 3 kwa kila nyumba.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameipongeza Wizara ya Afya kupitia Naibu Waziri wa Afya kwa kujibu vyema maswali na kwa ufasaha.

“Niwapongeze sana Wizara ya Afya kwa majibu ya moja kwa moja kwenye swali lililoulizwa” amesema Mhe Tulia Ackson

Previous articleWARATIBU WA IDSR NCHINI WAMETAKIWA KUZINGATIA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO
Next articleRAIS SAMIA ATEMBELEA KIWANDA CHA SC JOHNSON FAMILY KILICHOPO CHICAGO MAREKANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here